Saturday, June 30, 2012

HII NI AIBU KUBWA KWA WABUNGE WASIO NA MADEREVA

HII NI AIBU KUBWA KWA WABUNGE WASIO NA MADEREVA

 

habari kwa hisani ya francis godwin mzee wa matukio 

Spika wa bunge Anne Makinda
BAADA ya kushindwa kuwalipa madereva wao aibu nyingine yaibuka kwa kwa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni baada ya baadhi ya wabunge hao ambao walikuwa wakijiendesha wenyewe kudaiwa kuwatumia madereva wasio na sifa (madeiwaka) kuwaendesha pindi wanapokwenda bungeni kama njia ya kuficha aibu ya kujiendesha wenyewe.
Pamoja na wabunge hao kukwepa aibu hiyo ya kujiendesha bado baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakiongoza kwa kuwalipa fedha chini ya kiwango madereva hao wametishia kuwafukuza kazi madereva wao iwapo watatoa siri ya malipo kidogo wanayolipwa kwa sasa jamboleo jumapili limeelezwa.
Madereva hao wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa baada ya kutolewa kwa siri ya malipo ambayo wabunge hao wamekuwa wakiwalipa madereva ,wabunge hao wamekuwa wakiwatolea vitisho mbali mbali kwa madai kuwa malipo kidogo ambayo wanalipwa kwa sasa ni makubaliano ya wawili hivyo iwapo siri hizo zitavuja kwa vyombo vya habari basi watafukuzwa kazi .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotaja majina yao madereva hao walisema kuwa wabunge hao wameanza kutoa vitisho mbali mbali kwa madereva wao kwa madai kuwa iwapo watawataja majina wataharibu sifa kwa wapiga kura wao .
Alisema mmoja kati ya madereva hao kuwa iwapo wabunge hao wataendelea kuwapunja maslahi yao basi watakosa uvumilivu dhidi yao na badala yake watawaanika majina yao kama ambavyo walivyo kusudia kufanya hivyo kama njia ya kudai haki yao.
Kuwa kama wabunge hao watachukia na hatua hiyo basi watawaachia magari yao huko huo bungeni na wao kurudi majimboni kufanya kazi za kilimo badala ya kuendelea kutumikishwa bila malipo ya maana .
“Tunaomba wabunge wetu ambao ndio mabosi wetu kuwa na huruma na kuacha vitisho kwetu …kwani iwapo tutafanya kazi kwa kutishana sisi madereva ndio ambao tunaweza kuwatisha wao zaidi kwani siri zao zote tunazijua na hatutaki kuzitoa sasa ila kama watatumia jazba na kutufukuza basin a sisi tutaona ni vema liwalo na liwe tutawaanika”
Kwani alisema kuwa kwa kuwa sehemu kubwa ya madereva hao wanaopunjwa haki yao ni wabunge wanatokea katika majimbo husika iwapo mbunge atawafukuza kazi kwa wao kusema ukweli juu ya posho ndogo wanazowalipa basi watakwenda kuwashtaki kwa wapiga kura majimboni .
“Hata hapa tunavumilia tu kwani siri za wabunge sisi ndio tunaozitunza sasa wao kama watatanguliza hasira mbele badala ya utu sisi tutakwenda mwaga sumu majimboni kwani wakiwa majimboni wanajisifia kuwa wametoa ajira kwa vijana kwa kazi hiyo ya udereva wakati hawatulipi chochote”
Undani wa habari hii utausoma kesho katika gazeti la Jamboleo jumapili

No comments:

Post a Comment