ZAIDI ya viongozi 2000 wa makanisa ya Intenational Evangelism
kutoka kati nchi 5 wanatarajia kukutana jijini Arusha na kujadili changamoto
mbalimbali za nchi ya Tanzania
ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia za nchi,na hali ya maisha ya sasa kwa
watanzania
Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa Askofu wa
makanisa ya Intenational Evangelism Centre ya hapa nchini Bw Eliud Isangya
alisema kuwa viongozi hao watakutana jijini hapa wiki ijayo
Bw Eliud alisema kuwa viongozi hao watajadili mambo
mbalimbali ambayo kwa sasa yanaikabili sana nchi
ya Tanzania
ambapo changamoto hizo zinaweza kutatuliwa hata kwenye taasisi mbalimbali za
dini badala ya kutegemea zaidi Serikali kwa kila kitu
Alisema kuwa mara mbali na kuweza kutatua changamoto
mbalimbali ambazo zipo sana ndani ya jamii pia
watafanya maombi kwa ajili yan kuombea nchi ya Tanzania
pamoja na Zanzibar
dhidi ya machafuko ambayo yanatokea kila mara.
“kwa sasa zipo changamoto kubwa sana ikiwemo changamoto ya mabadiliko
ya tabia za nchi sasa kwa inawaasumbua wananchi wengi sana hasa wa vijijini
lakini kama taasisi mbalimbali zikiwemo za dini zitawaamasisha hata waumini
wake ni wazi kuwa jamii haitaweza kukumbwa na baa la ukame kwa maana hiyo
tutajadili masuala kama hayo ambayo yanaitesa jamii za watanzania walio wengi”aliongeza
Bw Eliud
Pia alisema kuwa taasisi mbalimbali za dini zinatakiwa
kusaidia jamii kwa kuweza kuwa bunifu na kubuni vitu ambavyo ni mzigo kwa
Serikali ili kuweza kuraisisha hata maendelo ya Miji na Majiji hapa nchini
‘kila siku wanasayansi wanabuni vitu vipya na vina uwezo wa
kuwasaidia jamii kwanini sisi kama wadau wa nchi hii tusiwe wabunifu wa kusadia
hata kuombea taifa katika majanga mbalimbali ambayo ni kikwazo cha maendeleo
tunataka tufanye hivyo ili kurudisha hata vitu ambavyo vimepotea kwenye nchii
hii ya Tanzania”aliongeza
bw Eliud
Mbali na hayo bw Eliud alizitaka Taasisi nyingine za dini
kuhakikisha kuwa kila mara zinayafanyia kazi changamoto ambazo zipo kwenye
jamii kwa kuwa wao ndio wana nafasi kubwa sana
ya kuweza kulikomboa taifa la Tanzania
mwisho
No comments:
Post a Comment