Chanzo: Arusha255 Blog
Sababu ya dosari hizo kwa binadamu ni maji yanayopatikana ndani
ya eneo hilo
yanayoelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha floride ambayo ndio inaaminika
kuharibu meno kwa kutengeneza tabaka la nje kuwa rangi ya ‘brown’ na kulainisha
mifupa, jambo linalopelekea mtu kuwa na matege.
Mamlaka ya Maji Arusha (Arusha Urban Water Supply Authority)
iliungana na wataalamu toka Chuo Kikuu cha University of Dar-Es-salaam kufanya
utafiti kuangalia kiwango cha kemikali ya ‘floride’ kilichomo kwenye vyanzo
vyake vya maji na kutafuta mbinu za kukabiliana nayo.
Mkurugenzi wa AUWSA, Injinia Ruth Koya alisema, Mji wa Arusha
una vyanzo vingi vya maji lakini vingi vina kiwango kikubwa cha floride na
wakati huo huo maji yakianza kuonekana kama
bidhaa adimu mjini hapa.
Kwa mujibu wa wataalamu, mtu anapoingiza mwilini kiwango kikubwa
cha floride humsababishia kupata ugonjwa unaojulikana kama
‘dental flourisis’ kwa lugha ya kitaalamu.
AUWSA imeshagawa tenda kwa ajili ya kununulia dawa za kuondoa
hiyo floride kwenye maji.
Wakati huo huo mtaalamu wa meno kutoka hospitali ya Saint
Elizabeth ya Arusha (SEHA), Anna William Msuya anasema matatizo haya ya meno
kwa wakazi wa Arusha mengine hutokana na kutokujua aina sahihi ya dawa za meno
zinazofaa kwa mazingira ya Arusha.
Alisema maji yanayopatikana Arumeru na Arusha mjini tayari yana
kiwango kikubwa cha madini ya floride na hivyo hakuna haja ya mtu kutumia tena
dawa ya meno yenye madini hayo. kufanya hivyo ni kufanya tatizo liwe kubwa
zaidi.
Anna anaeleza kwamba madini ya floride hupunguza kiwango cha
madini mengine aina ya calcium ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wameno imara
na mifupa kwa binadamu.
Mtaalamu huyu anawaasa pia watu wanaodhania wakitumia maji ya
viwandani wanaweza kuepukana na tatizo hili, na kuwakumbusha kuwa madini ya
floride hupatikana pia kwenye mboga za majani zinazolimwa maeneo tofauti ya
mji.
Kwa hiyo watu wa Arusha wanashauriwa kutumia zaidi dawa za meno
zisizo na flouride, na hasa zenye mjumuisho wa clacium ili kupunguza tatizo kwa
kiwango fulani.
Chanzo: Arusha255 Blog
No comments:
Post a Comment