.
IMEELEZWA kuwa kiasi
cha dola za Kimarekani Bilion 148huwa zinapotea ndani ya Nchi za bara la Afrika
kila mwaka kutokana na kuwepo kwa mianya mingi ya rushwa na badala yake fedha hizo zinapelekwa katika
nchi za Ugaibuni hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana kwa wananchi wan chi hizo.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Dkt Edward hosea wakati akizungumza katika
mkutano wa bodi ya ushauri wa masuala ya Rushwa kwa nchi za bara la Afrika
mapema leo jijini hapa
Aidha dkt Hosea alisema kuwa kiwango hicho cha fedha hupotea
kutokana na baadhi ya mianya ya Rushwa ambayo imo kwenye nchi hizo na badala
yake fedha hizo zinapelekwa kwenye nchi za Ugaibuni
Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo ya upotevu wa fedha
hizo unachangia kwa kiwango kikubwa sana
hata kukithiri kwa rushwa ndani ya Nchi hizo hali ambayo nayo inachangia hata
maendeleo duni ya nchi hizo za bara la Afrika
“hiki ni kiwango kikubwa sana
cha fedha ambazo zinapotea kusikojulikana lakini mpaka sasa tumeshaanza kuweka
mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa nchi za bara la Afrika hazikumbwi na
rushwa ingawaje pia changamoto ya kupambana nayo ni kubwa sana”Aliongeza Dkt Hosea.
Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa kwa Upande wa
Serikali ya Tanzania tayari
imeshaanza miachakato mbalimbali ya kujenga bodi ya kupambana na Rushwa ambapo
mchakato huo pia utasaidia sana kupunguza wimbi
kubwa sana la
Rushwa hapa nchini.
Dkt Hosea alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo la bodi hiyo ya
kupambana na rushwa utaaanza mara baada ya Kupitishwa kwa bajeti yake ambapo
jengo hilo
litajengwa ndani ya eneo la Kisongo mkoani Arusha
“kwa sasa tunafurai sana kwa kuwa ujenzi wa jengo hili
umeshawekwa katika mikakati na kitu ambacho tunasubiri ni bajeti yake na
tunachokiamini ni kuwa kupitia bodi hii tutaweza kuendelea kudhibiti mianya ya
rushwa ndani ya Nchi za bara la Afrika”aliongeza Dkt Hosea
No comments:
Post a Comment