Monday, June 11, 2012

LITA ELFU ZA GONGO ZAKAMATWA


HABARI NA UPAKO WA HABARI

JESHI la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kukamata lita elfu tisa za pombe haramu aina ya Gongo ambayo ilikuwa inayokea nchini Kenya na kuingizwa Tanzania kwa njia za Magendo

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha bw Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea June 10 majira ya saaa kumi na mbili za jioni katika eneo la Namanga

Alisema kuwa kufanikiwa kukamatwa kwa pombe hiyo haramu aina ya Gongo kunatokana na Taarifa kutoka kwa raia wema ambapo ndio waliotoa taarifa kwa jeshi hilo na jeshi hilo likaanza  msako maalumu

Kamanda huyo alisema kuwa mara baada ya taarifa hizo askari walirfanya doria ndani ya eneo hilo la Namanga  na walifanikiwa kumkamata raia mmoja wa kitanzania ambaye alijulikana kwa jina Nicoulaus Thobias(35) akiwa katika katika eneo hilo lita hizo za gongo ambazo zililkuwa kwenye mapipa 150

Aliendelea kusema kuwa mara baada ya kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo askari waliamua kufanya upekuzi katika gari lake na kumkumta na pombe hiyo haramu ambayo aliitoa nchini Kenya na kuileta Tanzania kwa ajili ya matumizi ambayo bado hajafahamika

“hapa mara baada ya kukamtwa askari hao walikagua gari alilokuwa nalo  mtuhumiwa huyo ambalo ni Scania  lenye namba za usajili  T 416 AJX ambalo linamilikiwa na Joseph Masawe ambapo mara baada ya hapo mtuhimiwa aliwekwa chini ya ulinzi’aliongeza kamanda Sabas

Pia alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipohojiwa juu ya pombe hiyo haramu alidai kuwa pombe hiyo Si pombe bali ni Spirit jambo ambalo halikuwa kweli na badala yake alikuwa anadanganya Polisi

Hataivyo Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika ambapo pia gari nalo bado linashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi

mwisho

No comments:

Post a Comment