Wanafunzi walemavu Mafinga waipigia magoti Serikali
Na Joachim Mushi, Thehabari.com- Mafinga
WANAFUNZI wenye ulemavu anuai katika Shule ya Msingi Makalala wameiomba
Serikali na wadau wengine kuwasaidia kuwajengea mazingira bora ya
kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu bora kama
ilivyo kwa watoto wengine.
Kauli hiyo imetolewa katika risala ya wanafunzi hao iliyosomwa jana
Wilayani Mafinga kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika
kiwilaya kwenye Shule ya Msingi Makalala nje kidogo ya Mjini wa Mafinga.
Katika maelezo yao watoto hao wameiomba Serikali na wadau wengine
kuwatizama kundi la watoto wenye ulemavu anuai kwa jicho la karibu, hasa
katika uboreshaji wa mazingira jumuishi ya kujifunzia katika shule zenye
watoto wenye ulemavu.
Pamoja na hayo wanafunzi hao walemavu wameomba kuboreshewa mazingira ya
lijifunzia katika Shule yao ya Makalala, ikiwa ni pamoja na kuwajengea
chumba maalumu kwa ajili ya kujifunzia kitakachokidhi mahitaji ya kundi
hilo maalumu.
Akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mafinga, Bi. Farida Mwasumilwe alisema licha ya Serikali
kujitahidi kuboresha huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu bado kuna
changamoto nyingi hivyo kuomba wadau kushirikiana kwa pamoja kuwasaidia
watu wenye ulemavu hasa watoto

Acheni Mafinga iitwe Mafinga duh!
Wadau jana nilikuwa Mjini Mafinga kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Afrika, nimejifunza kitu hivyo si vibaya
tushirikiane. Mara nyingi kilio cha wakazi wa Dar es Salaam na
vitongoji vyake ni joto linalowakera wengi karibia kipindi kirefu cha
mwaka, lakini kwa wanaokerwa na joto hilo si vibaya mnapokuwa mapumziko
(likizo) mtembelee Mjini Mafinga kupima baridi mwanana inayopatikana
eneo hilo kuanzia mwezi wa sita hadi wa nane. Leo baada ya mdau mkuu wa
mtandao wa Thehabari.com kuwasili Mafinga pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa Kituo cha Habari Kuhusu Walemavu (ICD), tulilazimika
kutafuta namna ya kuidhibiti baridi iliyokuwa ikivuma eneo hilo asubuhi
kabla ya kuendelea na majukumu mengine yaliyotuleta.
Nililazimika kuvaa hivi pamoja na mdau kutoka ICD
MAADAM RITAH AJITOLEA DAMU KATIKA KITENGO CHA DAMU SALAMA MJINI DODOMA
Majaji Maadam Ritah katikati Salama
Jabir kulia na Paoul wakiwa kazini wakati wa kusaka vipaiji vya Bongo
Star Search mjini Dodoma
Vijana wakionyesha vitu vyao mbele ya Camera wakati wa zoezi la kusaka vipaji vya washiriki wa Bongo Satr Search Mjini Dodoma
ZIARA YA NAPE KILOLO MKOANI IRINGA
Katibu wa Halmashauti Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa michezo mjini Ilula,
wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye akimpa msaada wa fedha Mwalimu Beatrice Luoga, wakati
alipozungumza na walimu wa mjini Mafinga, wilayani Mufindi mkoani
Iringa, juzi. Nape alimpa msaada huo kwa ajili ya kushughulikia
matibabu ya maradhi yanayomsumbua mwalimu huyo, na alizungumza na walimu
hao wa shule za sekondari na za msingi ili kujua changamoto
zinazowakabili na jinsi CCM iliyounda serikali inavyoweza kuyatatua.
Wananchi wa Kilolo wakimshangilia Nape baada ya kuzungumza nao kwenye Ofisi ya CCM, Kilolo.
Nape
akiwatuza wanakwaya wa CCM, Kilolo mkoani, Iringa walipoimba wakati wa
mapokezi yake wilayani humo. Kulia ni Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter
Msolla (Picha na Bashir Nkoromo BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment