Msaidizi
wa mbunge wa jimbo la Singida mjini na katibu mwenezi wa CCM manispaa
ya Singida Bw. Hassan Mazala (kulia), akimkabidhi Afisa wa idara wa
shule za sekondari jimbo la Singida mjini Bw. David Bulala jezi 300
zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam
Dewji. Wa kwanza kushoto ni katibu muhtasi wa Mbunge.
Msaidizi
wa mbunge wa jimbo la Singida mjini Bw. Hassan Mazala akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi jezi 300 kwa shule za sekondari za jimbo la
Singida mjini. Wa pili kulia ni Afisa wa shule za sekondari jimbo la
Singida mjini Bw. David Bulala na wa pili kushoto ni Katibu Muhtasi wa
mbunge.
Baadhi
ya jezi zilizotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh.
Mohammed Gullam Dewji kwa shule 20 za sekondari jimboni humo.
Na Nathaniel Limu
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa
vifaa vya michezo jezi jozi 300, zenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni sita kwa shule 20 za sekondari jimboni kwake.
Msaidizi
wa mbunge huyo Bw. Hassan Mazala amesema hayo wakati akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi jezi hizo, iliyofanyika kwenye ofisi ya
shirika lisilo la kiserikali la Saidia Singida yetu iliyopo mjini
Singida.
Amesema
jezi hizo zilikuwa ni sehemu ya msaada ambao ulikuwa utumike kwenye
ligi maalum ya kombe la 'Mo' ambayo shule zote za sekondari jimbo la
Singida mjini zingeshiriki.
"Lakini
baada ya ninyi kuandaa bajeti kubwa mno na wakati huo huo mbunge wetu
Dewji akikabiliwa na majukumu makubwa ya kutekeleza ahadi zake nyingi,
ligi hiyo tumeisitisha kwanza",amesema Mazala ambaye pia ni katibu
mwenezi wa CCM manispaa ya Singida.
Amesema
kwa sababu ligi hiyo tarajiwa maandalizi yake bado, sasa maamuzi ni
kwamba jezi hizo zitumike katika maandalizi ya michezo ya shule za
sekondari (UMISETA).Akifafanua zaidi, Mazala amesema wanafunzi na
vijana walio nje ya shule, wahamasishwe kupenda michezo ili pamoja na
mambo mengine, waweze kujijengea mazingira mazuri ya kujiajiri na
kuajiriwa.
Kwa
upande wake Afisa elimu taalum shule za sekondari manispaa ya Singida
Bw. David Bulala, alitumia fursa hiyo kumshukuru mbunge Dewji kwa
kuipunguzia ofisi yake makali ya gharama ya ununuzi wa vifaa vya
michezo.
HABARI KWA HISANI YA BLOGU YA FATHER KIDEVU
No comments:
Post a Comment