SERIKALI imeombwa kuboresha sera amabazo zitaweza kuinua
hali ya vijana wasio katika sekta rasmi ili ziwawezeshe kujikwamua kiuchumi sa
njari na kujiepusha na vishawishi mbali mbali wanavyokumbana
navyo.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa shirika la kimataifa la
maendeleo lisilo kla kimataifa (DSW)bw Peter Owaga alipokuwa akizungumza na vijana wakati wabunge wa Ujerumani walipotembelea miradi ya vijana
hao jijini hapa.
Bw Owaga alisema kuwa sera za kuwalinda vijana wasio katika
sekta isiyo rasmi ni muhimu kwa kuwa endapo itawekwa na kuboreshwa ni wazi kuwa
itasaidia kupunguza makundi ya vijana wanaozurura ovyo kutokana na kutopata ajira
“sekta iliyo rasmi ndio inayowatambua vijana wanaomaliza
vyuo vikuu lakini hawa walioko kwenye sekta iliyo rasmi hawatambuliki hali
inayopelekea vijana wengi kushawishika na anasa za dunia ,hivyo serikali a ikiboresha sera ya sekta iliyo rasmi ni wazi kuwa itawaondoa
kwenye umaskini”alisema Owaga
Alieleza kuwa sekta zisizo rasmi zikitengewa bajeti zitaweza
kuwasaidia vijana kujiepusha na mambo mbali mbali ambayo ndi chanzo cha
kuharibikiwa katika maisha yao.
Mbali na hayo alisema kuwa viongozi nao wanapaswa kuwekeza
kwa vijana na kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi mbali mbali ambazo
wamezikusudia kwa kuwa vijana wengi wanaumia kutokana na viongozi hao
kutotekeleza ahadi wanazozitoa kwa wakati muafaka.
“endapo kama ahadi ziatatekelezeka ni wazi kuwa vijana nao
watapata haki zao za msingi tofauti na sasa ambako ahadi zinatolewa tu kama
kawaida na hazitekelezwi hali inayowafanya vijana kuona kwa hawathaminiwi”alisema
Hata hivyo wabunge hao ambao wako ziarani hapa Tanzania
walisema kuwa wamefurahishwa na miradi ya
vijana hao walioko chini ya dsw kwa kuwa michango yao wanayoitoa
inawafikia walengwa ambao ni vijana hao.
mwisho
chanzo cha habari na upako wa ufalme
No comments:
Post a Comment