IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa
ya watu ambao ni maskini wanashindwa kuinuka katika umaskini na kuingia
kati hadhi ya utajiri kutokana na wao kujithaminisha sana na baadhi ya
mali zao huku wakishindwa hata kumpa Mungu Fungu la Kumi
Umaskini uliopo kwa sasa ni
fumbo kubwa sana baina ya watu na watu lakini chanzo kikubwa ni kutokuwa
na maagano na mungu, pamoja na kushindwa kutoa mafungu ya kumi.
Hayo yameelezwa jijini hapa na
Nabii Boniphace Malisa kutoka katika huduma ya Ukombozi ,Ministry for al
Nationals wakati alipokuwa akiongea na wakristo wa mji wa Arusha mapema
wiki hii.
Aidha Nabii Malisa alisema kuwa hakuna sehemu ambayo Mungu alisema wanadamu wawe maskini bali Mungu alisema kuwa wanatakiwa kutawala vitu vyote vya duniani hali ambayo inaonesha wazi kuwa Mungu aliweka maagano .
Alisema kuwa katika nyakati za
sasa asilimia kubwa ya watu wanalia kuwa wao ni maski ni bila kujua na
kutambua kuwa umaskini walio nao wamejitakia wao wenyewe hata kwa njia
ya kukiri na kukataa maagano na Mungu, pamoja na kutoa Mafungu ya kumi.
Alibainisha kuwa mkristo
anapotoa Fungu la Kumi ni wazi kuwa anarudisha matoleo na sadaka ambazo
amezipata kwa mungu lakini wanaoteswa na roho ya umaskini kwa sasa ni
wale ambao hawana mambo mbalimbali kama vile Imani, Maagano ya kimungu,
Mioyo ya kujitolea hali ambayo inatumika kama kigezo na Muovu shetani
hasa pale mtu anapodai haki yake
“leo unakuta mtu anadai kuwa
Mungu hamuonoi lakini ukiangalia hana hata agano lolote lile ambalo
ameliweka yeye pamoja na Mungu sasa Mungu atasimamaje lakini mtu
huyohuyo akienda kwa mganga anaweka agano na mganga Kwa Mungu
inashindikana je umaskini utaisha au utaongezeka mara dufu”alisema Nabii Malisa.
Pia amesema kuwa kanuni za
maagano ya Mungu ni za msingi kwa mtu yoyote yule ambaye anataka utajiri
kwa maana hiyo ni vema watu wakatafiuta maagano ya Kimungu na wala sio
maagano ya Kidunia(ZABURI 50.5)
Katika hatua nyingine amewataka
hata wale ambao wanaweka maagano dhidi ya Mungu kuhakikisha kuwa
wanawajibika Vema na kukumbuka maagano hayo kwa kuwa hata katika jamii
wapo baadhi ya watu ambao wanaweka maagano lakini wanashindwa
kuyatekeleza.
MWISHO
No comments:
Post a Comment