Wednesday, December 4, 2013

POLISI ARUSHA WASHIKILIA SILAHA ILIYOKUWA IKITUMIKA KWENYE MATUKIO YA UHALIFU



JESHI la Polisi mkoani Arusha,linashikilia silaha aina ya short gun
WINCHESTER  yenye namba za usajili c.056900 pamoja na mmiliki wake
ambaye alikuwa anaitumia kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu kwa mkoa
wa Arusha na nje ya mkoa wa Arusha

Pia Polisi mkoa wa Arusha ilifanikiwa kumkamata mmiliki wa silaha hiyo
ambaye ni Jumanne Abadlaha(25) maarufu kama babu G

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa
Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa silaha hiyo pamoja na jambazi
huyo walifanikiwa kumkamata September 27 majira ya asubuhi.

Sabas alisema kuwa Polisi waliokuwa katika doria waliweza kumkamata
jambazi huyo na silaha yake  katika eneo la Ungalmtd ambapo ndipo
makazi ya jambazi huyo mara baada ya kupewa taarifa na raia wema kuwa
anamiliki silaha kinyume cha sheria lakini pia anatumia kwenye matukio
mbalimbali ya uhalifu.

Aidha alidai kuwa mara baada ya kumkamata jambazi huyo na silaha yake
waliweza kugundua kuwa silaha hiyo tayari ilikuwa imeshakatwa kitako
lakini ndani ilikuwa na risasi 13

Sabasi aliendelea kwa kusema kuwa mara baada ya kumkamata jambazi huyo
pamoja na silaha yake waliweza kumuhoji na alikiri kuwa amehusika na
matukio mbalimbaliya uhalifu kama vile unyanganyi wa kutumia nguvu na
silaha, lakini pia anamiliki silaha hiyo kiyume cha sheria.

Pia alidai kuwa mbali na kuweza kugundua kuwa anamiliki silaha hiyo
kinyume cha sheria lakini pia silaha hiyo imekuwa ikitumika kwenye
matukio mbalimbali  ya uhalifu ambayo yameweza kutokea katika mkoa wa
Arusha na nje ya mkoa wa Arusha.

Hataivyo kamanda huyo amedai kuwa upelelezi zaidi bado unaendelea na
mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Wakati huohuo kamanda huyo aliwataka wakazi wa mkoa wa Arusha
kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa za siri hasa za wale wananchi wasio
waaminifu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu kwani matukio hayo ya
ualifu yamechangia sana kushuka kwa amani ya nchi ya mkoa wa Arusha.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment