Wednesday, December 4, 2013

HALMASHARI YAURARUSHA VIJIJINI WAFANIKIWA KUKUSANYA MILIONI 682 KUTOKA KATIKA VYANZO VYAKE VYA MAPATO


Wilaya ya Arusha Vijijini imefanikiwa kukusanya kiasi cha Milioni 682
sawa na asilimia 31.8 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ingawaje
kwa kipindi cha mwaka 2013,2014 wanatarajai kukusanya kiasi cha zaidi
ya bilioni mbili sanjari na kuibua vyanzo vya mapato ambavyo
vitaimarisha zaidi uchumi wa wananchi wake.

Hayo yamelezwa mapema jana na Kaimu mweka wa Halmashauri hiyo bw
Munguabela Kakulima wakati akielezea Vyanzo vya mapato ambavyo
vitakwenda sanjari na mpango wa matokeo makubwa (Big Result Now)kwenye
wilaya hiyo

Kakulima alidai kuwa kupatikana kwa fedha hizo kunatokana na jitoada
mbalimbali ambazo zinafanywa na idara yake ambapo ndipo zilipochangia
mafanikio hayo

Aidha alidai mpaka mwaka wa fedha wa sasa uweze kuisha wanatarajia
kuvuka hata lengo ambalo walikuwa wameliweka na hivyo kukusanya fedha
nyingi zaidi hali ambayo itachangia shuguli mbalimbali za maendeleo
kuweza kufanyika kwa haraka

Mbali na hayo alidai kuwa kwa sasa wanamikakati mbalimbali ya
kuhakikisha kuwa wanaweka uwezekano wa kubaini vyanzo vipya vya mapato
ambavyo navyo vitaweza kuweka halmashauri hiyo kwenye kiwango cha juu
sana

Mkakati mwingine ambao nao aliweza kuutaja ni pamoja na kuweza kuwapa
wananchi elimu ya kuweza kulinda vyanzo vya mapato lakini kuweza
kuonesha umoja baina ya watendaji wa halmashauri hiyo ili kuweza
kuharakisha shuguli mbalimbali za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri

Awali alisema kuwa pamoja na mikakati na jitiada ambazo zinafanywa na
idara ya fedha katika Halmashauri hiyo zipo changamoto ambazo nazo
zinachangia kukwamisha malengo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato
kutoka katika vyanzo

Kakulima alidai kuwa changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya wanasiasa
kuingilia shuguli pamoja na vyanzo vya mapato hali ambayo wakati
mwingine inasababisha waone kuwa halmashauri hiyo inachangia sana
kuwadidimiza.

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa ili matokeo ya
haraka yaweze kuja katika Halmashauri hiyo vyanzo vya mapato
vinatakiwa kulindwa lakini nao watendaji wa idara ya fedha wanatakiwa
kufuata wajibu wao wa kulinda na kuitetea halmashauri hiyo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment