Monday, December 16, 2013

VIJANA WA MERU WATAKAOKIUKA MAADILI NA KUIGA TAMADUNI ZA NJE YA NCHI KUCHAPWA VIBOKO 60 HADHARANI

VIJANA WA MERU WATAKAOKIUKA MAADILI NA KUIGA TAMADUNI ZA NJE YA NCHI KUCHAPWA VIBOKO 60 HADHARANI
 
Na Queen Lema, Meru
 
UONGOZI wa Kimila ujulikanao kama Rika la Kilovio kutoka katika kabila la Kimeru
 umepitisha sheria kali ya kudhibiti maadili kwa vijana wa kike na wa kiume hasa wale ambao wanaiga tamaduni  za mataifa ya nje ya nchi ambapo kwa kijana atakayebainika kuiga au kukiuka maadili ya Kitanzania basi atalazimika kuchapwa viboko 60 hadharani
 
Hatua hiyo inakuja mara baada ya baadhi ya vijana katika eneo hilo la Meru kuanza tabia ya kuiga tamaduni lakini hata madili ya mataifa ya nje hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa maadili kuendelea kuporomoka.
 
Hayo yameelezwa na Bw Akundaely Mbisse ambaye ni kiongozi wa marika ya vijana katika kabila hilo wajulikao kama “Kilovio”wakati wakimsimika na kumuingiza rasmi kiongozi wa vijana katika eneo hilo la Mareu Bw Herieli Mafie mapema jana.
 
Mbisse alisema kuwa utaratibu huo wa kuwapa vijana adhabu ya viboko 60 utaweza kurudisha maana halisi ya kijana wa kabila hilo ambapo kwa sasa jamii ya Mkoa wa Arusha bado inaonekana kuendelea kulelemewa na tatizo la vijana wengi kuiga tamaduni za nje ya nchi huku hali hiyo nayo ikichangia sana hata ubaribifu wa amani ya Kaya,hadi mkoa.
 
Alifafanua kuwa adhabu hiyo ya viboko 60 hadharani itaenda sanjari na vijana wote wenye tabia mbalimbali ambazo hazina tija kwenye jamii hiyo ya Meru kama vile Uzinzi, ulevi wa kupindukia saa za kazi, wizi, Mavazi yanaonesha maumbile,ukosefu wa adabu pamoja na makosa mengine ambayo chanzo chake ni kuiga maadili yasiyokuwa na tija kwennye jamii.
 
“tumejipanga kuhakikisha kuwa wilaya hii ya Meru inakuwa na utofauti wa hali ya juu sana kwani tunao uwezo wa kuwaweka vijana wetu wawe katika maadili mazuri, na masuala kama vile uvaaji wa nguo za ajabu utaisha na kwa hali hiyo jamii itaweza kupungza hata ujinga unaofanywa na baadhi ya vijana wachache huku wakisingizia umaskini’aliongeza Mbisse.
 
Hataivyo Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Arusha John Palangyo alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa maadili ya kila kabila kurudiwa ili kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao ya kila siku.
 
Palangyo alisema kuwa suala hilo la ulindaji wa maadili lina manufaa sana sio kwa vijana kwani hata kwa taifa kwani kwa sasa wapo baadhi ya vijana ambao wanaharib na kuvunja amani ya Nchi kwa kuwa hawana maadili ambayo yanaanzia ngazi za marika hadi taifa.
 
‘hili jambo la kuweza kuwaweka vijana katika mazingira mazuri ya kimaadili linawezekana kabisa na sisi watanzania tunatakiwa kuondokana na dhana potofu kuwa eti vijana wa sasa hawana maadili wa kuwafundisha maadili ni sisi wazee wa ukoo,rika, na hata wana siasa hivyo basi kila mtu anatakiwa kuzingatia hili lakini pia kuona kuwa kijana wa mwenzake ni wa kwake na hata kama ataharibikiwa basi atachangia uharibifu bila kujali anaharibu kwa nani”aliongeza Palangyo.
 
MWISHO

No comments:

Post a Comment