Tuesday, July 17, 2012

WILAYA ZA LONGIDO,NA KARATU ZAONGOZA KWA KUWA NA WANAWAKE WAJAWAZITO WENYE VIRUSI VYA UKIMWI WENGI.


CHANZO CHA HABARI Na Queen Lema, ARUSHA

Imeelezwa kuwa idadi ya wanawake wajawazito waliohudhuria vituo vya afya  kwa mwaka 2011  na kupima virusi vya ukimwi walikuwa 48375  ambapo kati yao 1677 walikuwa wameathirika na Ukimwi huku wilaya za longido na Karatu zikiwa zinaongoza kuwa na idadi kubwa sana kwa mwaka 2011 mkoani Arusha.

Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Arusha(Mount Meru) Dkt Omary Chande wakati akiongea katika mahojiano maalumu  na vyombo  vya habari mapema jana mkoani hapa.

Aidha Dkt Chande  alisema kuwa  walifanikiwa kujua na kutambua kuwa idadi hiyo ya wanawake imeathirika mara baada ya kufanya vipimo maalumu ambavyo vinafanywa kabla ya kufikia hatua ya uzazi ili kuepusha madhara ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.


“leo tunaweza kusema ,kuwa ndani ya wanawake hawa ambao wamefanikiwa kupimwa Ukimwi ambao ni kama asilimia 3 wameonekana kuathirika lakini ili kuokoa maisha ya mama na mtoto tulichokifanya ni kuhakikisha kuwa tunawapa elimu ya kujikinga na kuwalea watoto wao vema”aliongeza Dkt Chande.


Awali alisema kuwa zipo wilaya ambazo zinaongoza katika maambukizi ya Mama wajawazito ambapo Wilaya za Longido, na Karatu, na Manispaa ya Arusha zilionekana kukithiri kwa waathirika kutokana na kuwepo kwa migongano ya kijamii ambayo ndiyo chanzo kikubwa sana cha Magonjwa hayo

“hapa ukiangalia ndani ya Wilaya ya longido kuna maambukizi ya Ukimwi kwa kiwango cha asilimia 14, ikifuatiliwa na Karatu, kwa asilimia 4.7, huku nyingine ikiwa ni Manispaa kwa asilimia ni  asilimia 4 hali ambayo kwa kweli ni tishio kubwa sana lakini tunajikita sana kuhakikisha kuwa hawa watoto wanaozaliwa wanakuwa katika hali ya usalama zaidi”aliongeza Dkt  Chande

Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa mwaka 2011 pia watoto zaidi ya 928 walikutwa wakiwa na virusi vya ukimwi ambapo kati yao asilimia 82 walinyosnyeshwa maziwa ya mama zao ambapo asilimia 18 walikuwa wanatumia njia mbadala  ili kuendelea kuishi.

Pia alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwaka 2011 takwimu zinaonesha kuwa waki mama ambao wamejifungua hospitalini ni 33,643 ambapo kati ya hao 1907 hawakuwai kufika katika vituo vya afya wakati wakiwa wajawazito na hivyo hii kupelekea kuwepo kwa asilimia 6 ya wanawake ambao hawaeleweki kuwa kama wana maambukizi au hawana

Dkt huyo aliongeza kuwa kati ya hao asilimia 4 walikutrwa wakiwa tayari na maambukiz ya Ukimwi mara baada ya kupimwa huku wakiwa na ujauzito hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa changamoto hasa kwenye idara ya uzazi salama.

Hataivyo alitaja changamoto kubwa sana ambayo inaikabili idara lhiyo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa amasa ndogo sana ya wanaume  ambao wamekuwa wakijitokeza kupima virusi vya ukimwi wakifuatana na wake zao katika vituo mbalimbali vya Afya,

Alifafanunua kuwa changamoto hiyo imekuwa ikichangiwa na mambo mbalimbali ndani ya jamii za kitanzania ikiwemo ukosefu wa elimu kwa makundi hayo, mila na desturi zilizopo katika jamii mbalimbali,pamoja na  hali ya uchumi hivyo juhudi za lazima zinahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali katika kutoa elimu hiyo ili kuondokana na changamoto hizo


Mwisho

No comments:

Post a Comment