Wednesday, July 4, 2012

MTUME ARUSHA ADAI KUWA WAPO WAMILIKI, WACHUNGAJI,NA MAASKOFU WENYE HUDUMA KUBWA AMBAO WANAJIHUSISHA NA FREEMASONS ILI WAPATE FEDHA

HUYU NI MTUME HERBON AMBAYE ANA MAMBOZAIDI YA ELFU MOJA AMBAYO YANA HUSU MANABII WA UONGO NA VIONGOZI AMBAO WAPO KWENYE UTAWALA WA NGUVU ZA GIZA LAKINI WANATUMIA KOFIA YA YESU

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mtume mmoja wa jijini Arusha amesema kuwa kwa sasa zipo huduma kubwa za watumishi mashuhuri Tanzania ambao wanajihusisha na Nguvu za giza huku wakiwa wanatangaza Injili

Mtume huyo ambaye anatokea katika kanisa la Yesu ni bwana na mwokozi wa mataifa yote Bw Herbon Kisamo aliyasema hayo jana wakati akiongea na “UPAKO WA HABARI”mapema wiki hii jijini Arusha

Mtume huyo allisema kuwa Wamilikiu hao wa makanisa na wakuu wa huduma ambao wapo wengi sana na huku wengine wakiwa ni watu mashuhuri sana hapa nchini wanajiingiza kwenye ufalme wa Ki Freemasons ili waweze kupata fedha na waumini wengi sana

Aliongeza kuwa mpaka sasa ana ushaidi dhidi ya watumishi wa mungu wakubwa ambao wapo Kuzimu lakini wanaongoza ibada na kutoa ushuhuda wa uongo na bila kujua na kutambua kuwa wana mkasirisha sana Mungu

“hawa watumishi ambao wengine wanaonekana kama ni watumishi wa ukweli wanajiambatanisha na nguvu za giza na kisha wanatoa damu zao ili waweze kupata fedha na hata kwenye mitandao ya ki freemasons wanaonekana je hii ndio kazi ya Mungu kweli”alihoji Mtume huyo

Mbali na hayo aliongeza kuwa Mungu amempa ufunuo wa kuwasema hadharani wale wote ambao wanatumika kuzimu lakini wanashika biblia ya Mungu huku wakidai kuwa wanampenda na hatimaye wanawapeleka waumini wao kuzimu bila ya wao kujua

Alifafanua kuwa hapo awali alishawai kusema lakini Majeshi ya Kishetani ambayo yanaongozwa na watumishi hao yakaibuka lakini kwa kuwa ametumwa na Mungu hakuogopa hali kabisa

Alibainisha kuwa nao wakristo wanatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara wanajilinda na kuomba sana Uweza wa Mungu uweze kuwatala kwa kuwa wengi wamekufa macho ya rohoni na ndio chanzo cha kupelekwa kwenye utawala  mwingine wa giza

Aliongeza kuwa mbali na ,kuwa na macho ya rohoni pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuwachunguza zaidi viongozi wao kwa njia ya roho mtakatifu na pia kujua kweli ya Mungu

“wapo baadhi ya wakristo ambao kila mara wanakimbilia zaidi muujiza bila kujiuliza muujiza huo umetoka wapi na sasa hawa  ambao wanakimbilia zaidi muujiza ndio hawana ambao wanatekwa na mambo kama haya”aliongeza Mtume Hebron




No comments:

Post a Comment