Tuesday, July 17, 2012

ACHENI KUOMBA MAOMBI YA HASIRA DHIDI YA WALE WALIOJIBIWA




AMBAO  hawajibiwi maombi yao wametakiwa kuanza upya kuomba kwa kuwa wapo ambao hawajibiwi maombi yao kwa kuwa wanaomba maombi ya kukomoa na wala sio maombi ya unyenyekevu kama ambavyo Mungu aliagiza katika maandiko yake

Rai hiyo imetolewa na mchungaji Joseph Msengi alipokuwa akiongea  na waumini wa kanisa la FPCT Miembeni Usa River Wilayani Meru Mkoani hapa mapema wiki iliyopita

Mchungaji Msengi alisema kuwa watu wanatakiwa kujua jinsi ya kuomba kwa Mungu na hata kama maombi hayajibiwa hawapaswi kwenda kinyume cha mapenzi  kwa kuwa Mungu ana makusudio ya kila hitaji na kila ombi

“kuna watu ambao wanaomba maombi kwa kejeli mbele za Mungu na maombi ambayo wanayaomba ni maombi ya hasira kwa kuwa baadhi ya wengine pia wanaomba kwa kuwa baadhi ya majirani au ndugu zao  wamefanikiwa sasa je tunampangia Mungu kazi za kufanya jamani’aliongeza mchungaji huyo

Pia alisema kuwa kwa wale ambao hawajajibiwa wanatakiwa kuacha kuomba kwa hasira au kutoa maneno ambayo yanamfanya kazi za Mungu ziwe chini na badala yake wanatakiwa kuangalia ni yapi mapendekezo ya Mungu katika maisha ya kila siku ili maombi yajibiwe kwa haraka sana.

Hataivyo  aliongeza kuwa ni vema hata wakristo wakahakikisha wanafuatilia kwa karibu sana matakwa ya Mungu hasa kwenye biblia ambapo ndio muongozo wa maisha ya kila siku ingawaje kwa sasa biblia zinaoneka kubebwa kwa muda wa mara moja kwa wiki

‘jamani basi tuhakikishe kila sekunde na dakika tunaangalia mapenzi ya Mungu na kwa maana hiyo ukiangalia hata ndani ya makanisa yetu yeyote yule ambaye anafuatilia kwa karibu sana biblia hayumbi na imani wala haombi kwa hasira sasa kwa maana hiyo kwa nini tunaacha hili na kujiongoza wenyewe hii ni mbaya sana na ukiwa hivi utaoimba mpaka ‘alisema mchungaji Msengi.

Aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanajitafakari kwa kina na kuanza kuomba hata toba hasa kwa wale ambao wanaomba maombi ya hasira ya kulipizana mali na vitu vya kidunia kwani maombi ya hasira ndio chanzo pekee cha kushindwa kujibiwa

MWISHO

No comments:

Post a Comment