Tuesday, July 17, 2012

WILAYA YA MERU KUANZA KUWAPA VIJANA FURSA ZA KUIMARISHA UCHUMI WAO




WILAYA  YA MERU KUANZA KUWAPA VIJANA FURSA ZA KUIMARISHA UCHUMI WAO

WILAYA ya Meru Mkoani Arusha inatarajia kuanza kuwapa vijana wote wa Wilaya mbinu mbalimbali za kuweza kujikomba dhidi ya umaskini ambapo mbinu hizo zitachangia sana vijana kuacha kulalamika na kuona kama Serikali imewatenga huku wilaya hiyo ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zenye rasilimali nyingi.

Hayo  yamebainishwa wilayani humo na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Munasa Nyirembe wakati wa zoezi la kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Bi Mecy Silla mapema jana Wilayani humo

Bw  Munasa alisema kuwa mpaka sasa kuna kila dalili za kuweza kuokoa uchumi wa kijana wa Meru kwa kuwa vitenda kazi muhimu vikiwemo Ardhi vipo vya kutosha na kutokana na hali hiyo sasa Serikali imeshajiwekea utaratibu a kuhakikisha kuwa vijana wanaanza kunufaika mapema hivi sasa

Alifafanua kuwa mbali na hilo pia wilaya hiyo itaaza kwa kuwapa mawazo ya kijisariamali vijana wa maeneo hayo ambapo zoezi la kuwapa mawazo pia litaenda sanjari na zoezi la kuwakuzia zaidi Uchumi wao kwa kupitia fursa mbalimbali ambazo wanazo

“tunaamini kuwa hawa vijana wa hapa Meri wakipatiwa hata elimu ya ujasiamali basi wataweza kujikomboa na Maisha mabaya ambayo wengi wanaishi huku fursa nazo zikiwa ni nyingi sana na kutokana na hali hiyo basi tunataka kuona kuwa kila kijana anapiga hatua kwenye uchumi na mtu wa kuweza kuwasaidia ni sisi Serikali kwa kuwa hata wanapofanya maovu sisi ndio tunakuwa katika heka heka Sasa kila mmoja wetu akikishe kuwa anakuwa na mchanganua hata wa idadi ya vijana aliona na kisha aweze kufikiri  pamoja nasi”aliongeza Bw Munasa

Pia alisema ili kuendelea kuboresha zaidi maisha ya vijana ambao ni wazawa wa Meru kuanzia sasa wawekezaji wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaachana na tabia ya kutoa ajira kwa vijana wan chi za nje na kuaawacha vijana wa Kimeru wakiwa wanaranda randa Mitaani

Alifafanua kuwa kila muwekezaji ndani ya Wilaya hiyo anatakiwa kuanza utaratibu wa kuhakikisha kuwa vijana wananufaika na utendaji kazi wao na kutokana na hilo pia litachangia sana maendeleo na hata uchumi wa Wilaya ya Meru

“Nawasihi sana wawekezaji ambao wapo kwenye wilaya hii ya Meru kuhakikisha kuwa wazawa ambao ni vijana wananufaika na uwekezaji wao ni vema hata wakarudisha fadhila kwa vijana kwa kuwa wanapowachukua wafanyakazi kutoka nje ya nchi je hawa vijana waende wapi kama sio kuwaonea jamani”Aliongeza Bw Munasa

Awali aliye kuwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye kwa sasa ni mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  bi Mecy Silla alisema kuwa hilo linatakiwa kuchukuliwa kama changamoto  na watu wote ndani ya Wilaya hiyo kwa kuwa vijana ndio taifa la kesho.

No comments:

Post a Comment