Friday, July 20, 2012

MABALOZI WA NYUMBA KUMI KUMI WAHAMASISHENI WENYE WATOTO WALEMAVU WAJITOKEZE KATIKA SENSA



Na ROSE JACKOSON , Arusha

SERIKALI imeombwa kutoa elimu zaidi hasa kwa mabalozi wa nyumba kumi kumi maeneo ya Vijijini hasa kwa upande wa walemavu kwani baadhi ya wananchi wa vijijini bado wana uelewa mdogo kwa walemavu na hali hiyo huenda ikasababisha wasishirikishwe katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Hayo yameelezwa na Bi Yunisi Urasa ambaye ni Katibu wa shirikisho la vyama wenye ulemavu(SHIVYAWATA) mapema jana wakati akiongea na wakufunzi ambao watashirikishi katika zoezi la Sensa.

Aidha bi Yunisi alisema kuwa ni vema kama zoezi hilo liweze kuwafikia watu wote kama sheria inavyosema lakini wapo baadhi ya watu ambao hawataweza kufikiwa kutokana na uelewa mdogo , pamoja na Imani mbaya dhidi ya walemavu.

Aliongeza kuwa endapo kama Serikali kwa sasa ikiwashirikisha viongozi wa nyumba kumi kumi katika zoezi hilo la Sensa itachangia kwa kiwango kikubwa sana watu wenye ulemavu hasa watoto wa maeneo ya vijijini  kuweza kushiriki katika zoezi hilo la  Sensa.

 “kama tunavyoona ni kuwa zoezi hili linasonga mbele zaidi hasa hapa mijini lakini sisi tunajiuliza kuwa je Kijijini itakuwaje na kwa maana hiyo basi kama hawa mabalozi wa nyumba kumi kumi watahamasisha watu hasa wenye ulemavu watakuwa  ni kichocheo  kikubwa sana hasa kwa Serikali hasa kufikia kwenye malengo yake ya Sensa na watu kwa kipindi hiki”aliongeza Bi Yunisi.

Pia alisema kuwa mbali na Mabalozi kuhamasisha watu juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi hasa maeneo ya Vijijini  nao wanawake wana nafasi kubwa sana ya kusaidia na kuraisisha  zoezi hilo kwa kuachana na mila potofu za watoto walemavu kwa kuwa nao wana haki ya msingi kabisa.

“Wanawake wa Vijijini wanatakiwa kujua na kutambua kuwa Sensa ina umuhimu mkubwa sana kwa maendeleo ya jamii ambapo kupitia hata Sensa hiyo itaweza kusaidia Jamii hizo za Walemavu katika mahitaji muhimu ikiwemo huduma za Msingi kwenye maisha ya kila siku”aliongeza Bi Yunisi

Awali Mratibu wa zoezi hilo la Sensa kwa Mkoa wa Arusha Bi Magret Martin alisema kuwa mpaka wamejipanga kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii yanafikiwa katika zoezi hilo la Sensa kwa kuwa Sensa ina umuhimu mkubwa sana kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Bi Magret aliongeza kuwa ndani ya mafunzo yanayoendelea mjini hapa wamejipanga kuhakikisha makundi maalumu katika jamii nayo yanafikiwa na jamii kwa kuwa nayo yana nafasi kubwa sana katika kuraisisha zoezi hilo ndani ya jamii ya Kitanzania.

MWISHO

No comments:

Post a Comment