Tuesday, July 17, 2012

TUMIENI MBINU ZA KISASA ZAIDI KATIKA ZOEZI LA SENSA ILI MSIWE CHANZO CHA HASARA KWA SERIKALI- RC ARUSHA




CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA,ARUSHA

WAKUFUNZI  wa Sensa ya watu na makazi pamoja na wadau mbalimbali ambao watahusika katika zoezi la kuhesabu watu kwa mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu za kisasa zaidi ili kuwezesha zoezi hilo kufanikiwa kwa uraisi kwani kama halitafanikiwa litasababishia Serikali hasara kubwa sana.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo mapema jana wakati akifungua mkutano wa Wakufunzi wa Sensa kwa Mkoa wa Arusha

Bw Mulongo alisema kuwa endapo kama watalaamu hao watatumia utaalamu wao vizuri kutokana na mafunzo ambayo wameyapata basi wataweza kuokoa Serikali dhidi ya hasara mbalimbali ambazo zinaweza kutokea hasa pale zoezi hilo litakapokwama.

Alifafanua kuwa zoezi hilo lina umuhimu mkubwa sana na kwa hali hiyo ni vema kama watendaji wakuu wakawa makini kwa kuhakikisha kuwa wanakabiliana na Vikwazo ambavyo vinaweza kutokea wakati  wa zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi linaloanza hivi karibuni.

“kama zoezi hili litakwama ni hasara kubwa sana kwa Serikali na hata kwa maendeleo ya jamii sasa nawasihi sana ninyi wadau hakikisheni kuwa mnakuwa makini na kama mdau hanaona kuwa atakuwa moja ya kikwazo cha Sensa ni bora akasema mapema na ajitoe kuliko kuwa chanzo cha kushindwa kufikia malengo”aliongeza Bw Mulongo

Pia alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanachangia maendelo ya nchi hasa kwenye zoezi hilo la Sensa kwani Serikali inapojua idadi ya watu wake inaweza kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo ya Kijamii.

Awali Mratibu wa zoezi la Sensa kwa Mkoa wa Arusha Bi Magret Mutaleba alisema kuwa mpaka sasa maandalizi ya muhimu kwa ajili ya shuguli hizo za Sensa kwa Mkoa wa Arusha zimeshakamilika ambapo pia wanaendelea kutoa elimu kwa wahusika mbalimbali wa zoezi hilo ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.

Bi Magret aliongeza kuwa kwa sasa Wakufunzi  158 wanapata  elimu  juu ya kukabiliana na zoezi hilo ndani ya Mkoa wa Arusha ambapo wanatokea katika Halmashauri zote za jiji la Arusha na watapata mafunzo hayo kwa siku 12 huku lengo likiwa ni kuboresha zoezi hilo

“hawa Wakufunzi 158 ambao leo wamepewa mafunzo ni kwa ajili ya kuweza kuwapa na wengineo mafunzo ambapo na  wao watawapa watu kama vile makarani ambao nao watahusika katika zoezi hilo la Sensa na tunaamini kuwa kwa kutumian njia hii ya mafunzo basi itachangia sana kuraisisha zoezi hilo kwa uraisi zaidi”aliongeza Bi Magret


            MWISHO

No comments:

Post a Comment