NA JOSEPH LYIMO MANYARA
DIWANI
wa Kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara,Laurent Surumbu Tara (NCCR
Mageuzi) amekanusha vikali uvumi ulioenea wiki iliyopita kuwa amejiuzulu
udiwani baada ya kuhama chama hicho na kujiunga na Chadema.
Wiki
iliyopita katika Tarafa ya Bashnet na mji wa Babati kulienea habari kuwa Diwani
huyo ambaye pia aligombea ubunge mwaka 2010 na kubwagwa na Vrajilal Jitu Son
(CCM) ameondoka NCCR Mageuzi na kuhamia Chadema.
Akizungumza
jana na Mwananchi,Tara alisema hata yeye
alisikia hizo tetesi kuwa amejiuzulu nafasi hiyo ya udiwani baada ya kuondoka
NCCR Mageuzi na kujiunga Chadema jambo ambalo siyo kweli.
Alisema
huo ni mtazamo wa baadhi ya watu kuwa amehama chama chake na kujiunga na
Chadema hivyo kupoteza sifa ya kuwa diwani kitendo ambacho alidai kuwa
hakijafanyika.
“Hata
mimi nimesikia kwa watu wakisema kuwa nimejiuzulu udiwani kata ya Bashnet baada
ya kuondoka NCCR Mageuzi na kujiunga na Chadema,hayo ni maoni na mtazamo wao
hivyo nimeshawishika kukanusha hilo,” alisema Tara.
Alisema
kuwa bado anashikilia nafasi ya udiwani na hajafanya jambo hilo kwani endapo akifanya hivyo atatoa
taarifa rasmi na kutamka hadharani kuwa amejiuzulu nafasi ya udiwani wa kata ya
Bashnet kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.
Mwaka
2010 Tara aligombea nafasi ya udiwani na
ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini ambapo aliangushwa na mbunge wa sasa Jituson
lakini alikata rufaa Mahakama kuu akipinga kushindwa nafasi hiyo.
Pia,baada
ya kupeleka kesi hiyo Mahakamani,Jaji Fatuma Massengi aliisikiliza na kutupa
vipingamizi vyote alivyovitoa kwenye ushahidi wake ili Jituson afutiwe ubunge
lakini alifikisha kesi hiyo Mahakama ya rufaa kupinga maamuzi hayo.
Hata
hivyo,Majaji watatu waliosikiliza rufaa yake waliipinga na kudai kuwa Jituson
alishinda ubunge kihalali hivyo ataendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo hadi mwaka 2015 na Tara
anatakiwa alipe gharama za uendeshaji kesi hiyo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment