TUNATAMBUA
MCHANGO WA SEKTA BINAFSI-SERIKALI
Na Mustapha leo,ARUSHA
SERIKALI imesema
inatambua na kuthamini mchango wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo
yamekuwa yakisaidia kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini ambako
wananchi wamekuwa hawapati huduma ya moja kwa moja kutoka serikali.
Hivyo mashirika
hayo ni mbia mwenza wa serikali katika kutoa huduma na serikali itaendelea
kushirikiana nayo kwa ukaribu lengo ni kuwafikishia wananchi huduma mbalimbali
ili waboreshe maisha yao
Rai hiyo imetolewa
jana na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,bi Evereen Itanisa, alipokuwa
akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS) na
uongozi wa serikali mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Olasit Garden, jijini
Arusha.
Itanisa,aliongeza
kuwa hadi kufikia mwaka 2012 kuna mashirika yasiyo ya kiserikali 3600
yamesajiliwa hapa nchini ambapo mkoa wa Arusha una mashirika 385 ambayo
yamekuwa yakifanya kazi nzuri za kuhudumia wananchi katika maeneo ambayo hasa
huduma za moja kwa moja kutoka serikalini hazipo na mashiriuka hayo yamekuwa ni
mbia katika maendeleo.
Alisema wilaya
ya Ngorongoro ina mashirika 15, Karatu 15, Longido 21, Meru 52 , Arusha DC,
64 Monduli 52 na jiji la Arusha 166 .
Pia aliongeza
kuwa hali hiyo imeyafanya mashirika hayo kuwa mkono wa pili wa serikali katika
kufikisha huduma bora kwa wananchi hivyo serikali itaimarisha mahusiano na
mashirika hayo katika kuwahudumia wananchi waweze kupata huduma stahiki..
Alisema kutokana
na wingi huo wa mashirika hayo serikali ilitumnga Sera, Sheria na kanuni ambayo
ndio mwongozo wa utekelezaji na usimamiz wa majukumu ya mashirika hayo ili
kuboresha mahusiano kati ya serikali, jamii na wananchi
Itanisa alisema
kuwa kutokana na hali hiyo lazima mashirika hayo yafanye kazi zake
kwa kuzingatia utekelezaji wa wa Dira ya taifa, ya maendeleo na mpango wa taifa
wa miaka mitano mpango mkakati wa mkoa na halmashauri ya Jiji na
wilaya
Amesema lengo la
mkutano huo ni kufahamiana, nani anatoa huduma zipi na eneo lipi,
kuwezesha kupitia kwa pamoja Sera, Sheria na Kanuni za mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali na vyombvo vlivyoundwa vya kusimamia utendaji
kazi kwa mashirika hayo,pia kupitia taarifa za utekelezaji sanjari na
kuangalia changamoto zinazoyakabili mashirika hayo.
Awali katibu
tawala msaidizi Mipango na Uratibu, Anza _Amen Ndossa, amesema kuwa lazima
mashirika yote yafuate Sera na mwongozo wa serikali namna ya kufanya kazi
na kuondoa migongano kati yao
kwa kutoa huduma za aina moja katika eneo moja.
Amesema
mashirika hayo yana kabiliwa na changamoto nyingi na mkutano huo unalenga
kukimarisha mahusiano kati yao na serikali na kuondoa migongano kati yao na
kupitia mkutano huo mashirika hayo yataelewa mipaka na majukumu yao na kutoa
taarifa za utekelezaji wake kwa wakati bila kigugumizi pia mkutano huo utajenga
kuaminiana kati ya Serikali na mashirika hayo..
Ndossa,
akawakumbusha maafisa Maendeleo ya jamii kila halmashauri kuwa wanalo
jukumu kubwa la kushirikiana na mashirika hayo kwa kuyapangia maemneo ya
kufanyia kazi ili kuondoa muinginiliano inayosababisha kukwama kwa miradi
iliyokusudiwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment