SITALIPIZA VISASI KWA MTU YOYOTE YULE-DKT KIKWETE
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiombewa dua na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro leo Novemba 15, 2012
tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha
Na Queen Lema, Arusha.
KAMWE SITALIPIZA VISASI-Dkt Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete, amesema hawezi kulipiza visasi kwa watu
wa aina mbalimbali wakiwemo watumishi wa serikali ambao hawaelewani nao bali
watumishi wote watahukumumiwa kwa majungu yao ndani ya jamii.
Rais Kikwete ameyasema hayo , jana
jioni kwenye uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) alipokuwa akizungumza na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini
mkoa wa Arusha, waliofika
kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa CCM kwa kipindi
kingine cha miaka mitano ijayo, alipowasili tayari kwa ziara ya kikazi
mkoani Arusha.
Rais, amesema sio kweli kwamba watumishi wote serikalini ni
marafiki zake la hasha bali wapo wengine sio marafiki lakini wanafanya kazi
kutokana na sifa na uwezo wao na hivyo kila mmoja atahukumiwa kwa majukumu yake
Amesema hana moyo wa chuki
na mtu yeyote na kamwe hawezi kulipiza kisasi hata kama walivurugana
kipindi kilichopita na akasisitiza kuwa watumishi wote watahukumiwa kwa
majukumu yao tu
Akawataka watumishi wote kutimiza majukumu yao ipasavyo na
kuwaonya watakaovuruga atawashughulikia
Kuhusu utekelezji wa ahadi mbalimbali rais, amesema
atajitahidio kuzitekeleza ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake
kilichobakia na endapo kama hazitakamilika zote basi rais ajaye atazitekeleza
Kuhusu ujenzi wa madaraja amesema serikali ya awamu ya
kwanza iliweza kujenga daraja la Mto Kirumi lililopo wilayani Tarime, katika
mto Mara, na serikali ya awamu ya tatu ilijenga Daraja la Mkapa, na sasa
serikali yake inajenga madaraja mbalimbaIi yakiwemo mto Malagarasi, Kilombero, na maeneo mengine
nchini na tayari makandarasi wameshakabidhiwa kazi hizo
Aliongeza kuwa viongozi hao wa dini kuiombea amani Tanzania na
kueleza kuwa iwapo amani itatoweka kila kitu kitavurugika na maswala yote ya
maendeleo yatakuwa hayapo tena.
Kwa upande wao viongozi hao weameahidi kuipa ushirikiano
serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Dkta Jakaya Kikwete na kuahidi
kuendelea kuomba amani ya nchi idumu.
Wamesema, asijali kelele na kebehi na shutuma zinazotolewa na
baadhi ya watu bali aendelee kutekeleza majukumu yake na kazi zake alizozifanya
zinaonekana na ndizo zitawasuta wote wanaomshutumu.
Wamerejearea kauli ya Yusufu Makamba, aliyoitoa hivi
karibuni katika mkutano mkuu wa CCM ulionmalizika mjini Dodoma na kusema kuwa
rais sio malaika hivyo asihukumiwe bila sababu bali ahukumiwe kwa kazi
alizozifanya wala asihukumiwe kwa
matendo ya watoto wake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment