Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa serikali ipo
kwenye mchakato wa kuhakikisha vituo vya afya na zahanati hapa nchini
vinajengwa kwenye vijiji, kata ,wilaya na kwamba hospitali za mkoa zinakuwa na
hadhi ya rufaa.
Rais Kikwete ameyasema hayol eo wakati akizindua hospitali teule ya Olturumenti kuwa ya wilaya, ambapo hapo
awali ilikuwa kituo cha Afya katika halimashauri ya wilaya ya Arusha,na kutoa
wito kwa vituo vya afya na zahanati zilizopo kuboreshwa ili ziwe na hadhi ya
kulaza wagonjwa.
Aidha alisema utekelezaji
wa mpango wa mpango huo umeanza na unalengo la kuwasogezea huduma za Afya wananchi kwa ukaribu na kuondokana na adha inayowakabili ya kufuata huduma hiyo
umbali mrefu .
Alisema katika kukamilisha
mpango huo serikali imeongeza mara sita bajeti yake kutoka shilingi bilioni 271
ya mwaka 2005 na kufikia kiasi cha shilingi Trioni 6.2 ,ambapo lengo ni
kuhakikisha kuna kuwepo na vituo vya Afya na zahanati za kutosha hapa nchini.
Hata hivyo aliwataka
viongozi husika akiwemo waziri wan chi ofisi ya rais dkt Hawa Ghasia kuzifanyia
kazi changamoto zote zinazozikabili hospitali vituo vya Afya na zahanati ili
kuhakikisha vinatoa huduma iliyo bora itakayo saidia kupunguza kero kwa
wananchi.
Kikwete aliongeza kwa
kusema kuwa serikali imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na maambukizi ya
malaria kutoka asilimia 14 na kufikia asilimia 2 ,sanjari na kuweka mipango mikakati
mbalimbali ambayo inalenga kuimarisha zaidi afya ya Mtanzania dhidi ya
maambukizi ya ugonjwa huo
Alitaja Mikakati hiyo
ambayo inaendelea kutekelezwa ili kuepusha jamii na maambukiz mapya ya ugonjwa
wa Malaria kuwa ni pamoja na kugawa vyandaru viwili kwa kaya,ambapo hadi sasa Jumla ya Vyandarua Milioni 13
vimeshagawiwa,huku mkakati mwingine ambao unafuatwa ni kupuliza dawa kwa kila
kaya,na mkakati mwingine ni kujenga na
kuimarisha zaidi kiwanda ambacho kinazalisha Viluilui ambao wataweza
kushambulia wadudu wa Malaria.
Awali mganga mkuu wa
Halmashauri ya wilaya ya Arusha Thobias Mkina alisema kuwa pamoja na kuwa
Ujenzi wa hospitali hiyo ya Oltument umegarimu kiasi cha zaidi ya Milioni 924 lakini bado kuna
changamoto lukuki ndani ya Hospitali hiyo ambayo inatarajia kuhudumia maelfu ya
wakazi wa wilaya hiyo na nyingine za jirani.
Dkt Thobias alitaja
changamoto kubwa sana ndani ya hospitali hiyo kuwa wa majengo ya kutosha hasa
wadi za wamama wajawazito, watoto , chumba cha X ray, pamoja chumba cha kupimia
magonjwa ya VVU hali ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa haraka sana ili kuweza
kuboresha afya za wananchi wa wilaya hiyo
No comments:
Post a Comment