MBOWE ACHANGISHA MILIONI KUMI KWA AJILI YA UJENZI WA MABWENI
YA SHULE YA OLOKII,AWASHUKIA WANASIASA WANAOENDEKEZA ITIKADI ZAO HADI KWENYE
MAKANISA NA MICHANGO YAKE
Na Bety Alex, MERU
MWEYEKITI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA)Freeeman mbowe amewataka wanasiasa kuachana na tabia ya
kupeleka itikadi zao za kisiasa hadi ndani ya makanisa kwa kuwa itikadi hizo za
kisiasa zinaonekana kushamiri hata kwenye baadhi ya makanisa na hivyo kunyima
maendeleo ingawaje wanasiasa hao wana nafasi kubwa sana ya kuchangia
Mbowe aliyasema hayo wiki iliyopita katika harambee maalumu
ya kuchangia mabweni ya shule ya Ufundi yaOlikii ambayo ipo chini ya kanisa la
KKKT Dayosisi ya kaskazini kati ambapo pia katika harambee hiyo jumla ya
Milioni 10 ziliweza kupatikana
Alisema kuwa inashangaza sana
kuona kuwa baadhi ya wanasisasa wanashindwa kuchangia shuguli mbalimbali za
maendeleo ya kanisa au kushiriki hata kwa pamoja katika kuchangia michango au
kuendesha harambee kwa kuhofia kukutwa na Mwanasiasa mwingine jambo ambalo kama
litaendelea hivyo basi litasababisha kabisa maendeleo ya kanisa kuwa hafifu sana
Aliongeza kuwa wanasisa wanapswa kujua na kutambua kuwa ni
wajibu wao hata kuhakikisha kuwa wanakuwa sehemu ya kanisa kwa kuweza kuendesha shuguli mbalimbali za
maendeleo hasa katika ujenzi wa makanisa pamoja na mambo ya msingi ambayo
yanafanywa na kanisa la leo ambapo kwa sasa bado hali ya kiitikadi inaendelea
kushamiri ndani ya makanisa
Alifafanua kuwa hali hiyo pamoja na kuwa si njema sana kwa maendeleo ya kanisa kama itaendelea hivyo
itasababisha kasi ya kumjua Mungu hasa
katika siasa hizo itapungua sana na badala yake
kasi hiyo itaelekezwa zaidi katika mapabano ambayo hayana maana huku mapambano
hayo huenda hata yakasabisha sana
baadhi ya watu kukosa Amani dhidi ya wanasiasa hao
“inashangaza sana leo mimi kama Mbowe nikionekana mahala
hapa ambapo ni patakatifu basi mtu wa CCM haji wala hashiriki kabisa sasa je
tunajenga taifa la Kichadema au Ki CCM hapa na hali hii si hali ya kuendelea
kuingalia kwa macho yetu bali hali hii inatakiwa kuangaliwa hata na viongozi wa
dini wasimame vizuri na hata ikiwezekana waombe si jambo zuri kwani kama ni Siasa basi zisiingizwe itikadi
hadi ndani ya makanisa yetu kwani pia hali hiyo inasababisha tuyabomoe na wala
sio kuyjenga;’aliongeza Mbowe
Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wanasiasa ambao
wanangangani itikadi za kivyama wanapaswa kujua na kutambua kuwa kamwe
hawapaswi kufunga ndoa na vyama vya kisasa bali wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanakuwa wazalendo wa vyama vyao na kamwe itikadi kati ya CCM na Chadema
isisababishe wakashindwa kutumikia Taifa hasa kwa Upande wa Makanisa yao.
Awali Meneja wa Shule hiyo ya Sekondari na Ufundi ya Olikii
Mchungaji Izack Kisiri alisema kuwa lengo halisi la kufanya Harambee hiyo
ambayo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Zaidi ya Milioni 10 ni kuendeleza
Mabweni kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuimarisha zaidi elimu
Mchungaji Kisiri alisema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa
kupata zaidi ya Milioni 10 lakini bado shule hiyo ina hiuitaji mkubwa sana wa
mabweni kwani endapo kama kutakuwa na Mabweni ya kutosha basi itaweza kuongeza sana hata kiwango cha
elimu hasa katika eneo hilo la Olokii
ambalo bado lina uhitaji mkubwa sana .
‘tunafikiria kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 250 kwa
ajili ya ujenzi wa mabweni mawili lakini kwa awamu hii ya kwanza tunashukuru
Mungu tumepata hii Milioni 10 lakini tunawatia Moyo wakristo na wadau wengine
wa elimu kuhakikisha kuwa wanatuunga mkono na kuweza kuimarisha elimu hasa kwa kuwa na mabweni imara”aliongeza Mchungaji Kisiri.
Awali Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri mkoani hapa(
KKKT)dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt Thomas Laizer alisema kuwa ni jambo la
ajabu sana kwa wanasiasa kuchukiana ovyo kwa kuwa siasa inaenda kama mchezo wa
mpira ambao kamwe hautabiriki na hivyo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea
tabia ya kupenda na kuthaminiana wao kwa wao hasa kwenye majukumu ya msingi ya
Kimaendeleo.
Dkt Thomas alisema kuwa wapinzani kuwakataa watawala na
watawala kuwakataa wapinzani si jambo jema na halitakiwi kuendelezwa kwa sasa
kwani wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa kitu kimoja na kutatua matatizo
mbalimbali ambayo yanaikabili jamii kwa
sasa likiwemo suala zima la uvunjifu wa amani ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment