WALIOKUWA MADIWANI WA CHADEMA WALIPISHWA FAINI YA MILIONI 15
NA MAHAKAMA WAKISHINDWA KULIPA KWENDA MAGEREZA
NI KWA KOSA LA KUKIUKA TARATIBU ZA CHADEMA NA KUINGIA KWENYE
VIKAO VYA KUMTAMBUA MEYA WA CCM
Na Queen Lema,Arusha
HATIMAYE hukumu ya kesi ya madai iliyokuwa ikiwakabili waliokuwa madiwani watano wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)
hukumu yake imesomwa ambapo mahakama imeamuru madiwani hao kulipa kiasi cha
shilingi milioni 15 kwa awamu mbili na endapo kama
watashindwa kulipa fedha hizo basi watapelekwa magereza
Akitoa hukumu hiyo mbele ya Umati wa watu ambao walikuwa
wamefurika mahakamaani hapo mapema jana katika mahakama kuu kanda ya Arusha Charlz
Magesa alisema kuwa rufaa imefika mwisho
Magesa alisema kuwa washitakiwa hao ambao walikuwa madiwani wa kata tano za jiji la
Arusha wamekutwa na hatia hivyo mahakama imeamuru walipe kiasi hicho cha fedha
haraka iwezekanavyo na endapo kama watashindwa
kufanya hivyo basi watachukuliwa hatua kali ikiwemo kupelekwa magereza.
Aliongeza kuwa kwa sasa Madiwani hao wanatakiwa kulipa fedha
hizo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ndani ya wiki mbili wakati
awamu ya pili itakuwa ya mwisho na nibaada ya miezi miwili.
‘kwa sasa mnatakiwa muhakikishe kuwa mnalipa fidia kwa
haraka sana na kama
mtashindwa kufanya hivyo basi mahakama itachukua hatua na maambuzi makali zaidi
ya haya’aliongeza Magesa
Wakiongea nje ya mahakama mara baada ya kukubaliana kulipa
kiasi hicho cha fedha madiwani hao ambao walikuwa mahakamani hapo ambao ni
Rehema Mohamed,Charlz Mpanda,na Rubeni Ngowi walidai kuwa Chadema haiyawatendea
haki kwa kuwa fedha ambazo wanatumia kumlipa Wakili ili kuwakandamiza ndizo
walizozitafuta kwa kipindi cha hapo awali.
Madiwani hao waliongeza kuwa wao wapo tayari kulipa hizo
gharama kwa ndiyo haki ambayo Chadema walikuwa wanaililia hivyo wameomba
Viongozi wa Taifa watafute njia nyingine ya kutatua migogoro na wala sio
kufukuza kwani inapoteza imani na chama
‘ukiangalia hapa tunaambiwa kuwa tulipe kiasi hiki cha fedha
lakini nguvu zetu bado hazijalipwa na sisi ndio tuliotangaza Chadema kwa mkoa
wa Arusha na mpaka sasa Kila mtu anaijua Chadema lakini malipo yake ndiyo haya
sisi tunasema kuwa huu si mwisho wa siasa bado tupo na tutakutana katika gemu
nyingine ‘waliongeza madiwani hao
Pia walisema kuwa pamoja na kuwa baadhi ya waliokuwa
madiwani hawataki siasa lakini bado wengine wataendelea tena kwa kishindo
kikubwa hata kama Chadema wanadai kulipwa fedha zao na kata zao zikiwa zinabaki
hazina madiwani kwa muda mrefu sana.
Awali Kesi hiyo ilitokana na madiwani hao kufungua kesi ya
kupinga kufukuzwa na kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka sheria na
kanuni za chama, zikiwemo sheria za kuwataka kutoingia katika vikao vya
madiwani vya Jiji la Arusha kwa madai ya kutomtambua Meya wa Arusha Gaudence
Lyimo wa Chama cha Mapinduzi(CCM)
No comments:
Post a Comment