MAJESHI YA SADC KUENDELEA KUTOA MSAADA KWA NCHI ZENYE
MAJANGA,NA VITA
Na Queen Lema,ARUSHA
UMOJA wa nchi zinazoendelea kusini mwa jangwa la Sahara(SADC)umesema kuwa utaendelea kupeleka majeshi kwenye nchi zenye mitafaruku
mbalimbali yakiwemo majanga na vita huku lengo likiwa ni kuepusha vifo.
Kauli hiyo imetolewa jana(Leo)na Kanali Gerson Sangiza
ambaye ni mkuu wa kitengo cha ulinzi na mipango katika sektetarieti ya SADC
wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mipango mbalimbali ya
majeshi ya umoja huo
Kanali Sangiza alisema kuwa kwa nchi zenye majanga
mbalimbali yakiwemo majanga ya vita,mitetemeko,pamoja na mafuriko ambazo ni
wanachama wa umoja huo wataweza kusaidiwa kwa kupewa misaada na majeshi ya nchi
kama kumi na tano
Alifafanua kuwa kupitia umoja huo wa majeshi kuweza kusaidia
nchi zenye majanga kutaweza kuepusha nchi nyingine ambazo zipo jirani kupata
matatizo mbalimbali ambapo kupitia matatizo hayo nayo yanachangia sana kukitihiri kwa
majanga.
‘kama sisi SADC hatutashirikiana kwa pamoja katika kutetean
amani ya nchi yenye vita kupitia kwenye majeshi yetu ni wazi kuwa matatizo
mengi sana yataweza kuibuka kama vile vifo na hata wakimbizi,ingawaje kama kuna
matatizo tukishirikiana kwa pamoja ni wazi kuwa tutaweza kuleta amani tena ya kudumu na hiyo itafanya madhara mbalimbali ndani ya
nchi yenye vita kukoma kabisa”aliongeza kanali huyo
Pia alisema kuwa mbali na kudumisha amani ndani ya nchi
zenye vita pamoja na majanga mbalimbali kupitia umoja wa majeshi hasa ya nchi
hizo za SADC majeshi hayo yanamikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa ndani ya
karne ya sasa na karne ijayo hakuna mapigano ambayo ndiyo yanayochangia sana kukithiri kwa vita.
Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa Majeshi ya
nchi 15 yanafanya kazi kwa umoja mkubwa sana
hasa kwa kusaidia nchi znye vita na majanga lakini bado wana mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha kuwa kila Nchi mwanachama wa Umoja huo pamoja na
majeshi yake yanakuwa katika viwango ambavyo vinahitajika
Alisema kuwa Mikakati hiyo ni pamoja na kubadilishana uzoefu
baina ya Nchi na nchi ambapo hali hiyo inasaidia Vikosin mbalimbali vya Jeshi
kuweza kufanya kazi kwa uzoefu wote ambao wao kwa wao wanaujua na hivyo
kurahisisha kazi hasa pale inapotokea hasa ya Majanga, na Vita.
“kwa mfano hapa kwetu Tanzania tuna chuo cha TMA kipo
Monduli pale wanajeshi kutoka Nchi mbalimbali wanasoma na kuendelea kujifunza
mbinu mbalimbali lakini na sisi wanajeshi wetu pia na wao wanakwenda sehemu
mbalimbali kujifunza nah ii inachangia sana kuweza kuwaandaa kuwa tayari kwa
nyakati zozote zile’alisema
MWISHO
No comments:
Post a Comment