PUNGUZENI
IDADI YA MBWA MITAANI KWA KUWAFUNGA VIZAZI
Na
Queen Lema,Arusha
WAFUGAJI
wa Mbwa kwa mkoa wa Arusha wametakiwa kuwafunga Mbwa wao vizazi ili kuweza
kupunguza wimbi kubwa la Mbwa ambao wanazagaa ndani ya Mitaa huku baadhi ya
Mbwa hao wakiwa na Ugonjwa wa kichaa,hali ambayo inafanya madhara ya Ugonjwa
huo kwa Jamii kuwa makubwa zaidi.
Hapo
awali Serikali ilikuwa inapunguza idadi ya Mbwa kwa kuwapiga Risasi lakini njia
hiyo si nzuri sana
kwani inawafanya wanyama hao kukosa haki ya kuishi kinyume cha Sheria na haki
za wanyama duniani.
Hayo
yamebainishwa Mjini hapa na Bw Livingstone Masija ambaye ni Mratibu wa Mradi wa
chama cha kulinda na kutetea haki za wanyama mkoani hapa(ASPA) wakati akiongea
na wakazi wa Kijiji cha Nadosoito kuhusu umuhimu wa kufuata sheria ,kanuni,haki
na taratibu za wanyama hasa Mbwa wa mkoa wa Arusha.
Alisema
kuwa ndani ya Mkoa wa Arusha hususan Manispaa ya Arusha kuna ongezeko kubwa sana la Mbwa ambao wanazagaa Mitaani huku Mbwa hao wakiwa
hawana makazi rasmi hali ambayo ni hatari sana
kwa Afya za wana jamii hasa watoto ambao mara nyingi sana
wanaonekana kupenda Mbwa kwa ajili ya michezo yao
Alifafanua
kuwa ili kuweza kupunguza kasi ya Mbwa hao kuzaliana na kuongezeka mara kwa
mara basi wamiliki wa Mbwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawafunga vizazi Mbwa
hao ili wasiweze kuzaliana ovyo na kuendelea kusababisha madhara makubwa sana
kwa jamii ambayo kila mara inapata matatizo kutokana na Ugonjwa huo wa kichaa
cha Mbwa
“kama
wamiliki au wafugaji wa Mbwa wataendelea kuwaachia Mbwa wao wazaliane Ovyo
mitaani basi watakuwa ni sababu mojawapo ya kusababisha hata vifo vya watu
ambao hawana hatia kwa kwua hawa mbwa wanapochanganyana na mifugo mingine ni
raisi sana kuwaambukizia vichaa lakini kama wapo wachache itakuwa ni raisi sana
kuweza kuwaweka chini ya Uangalizi wa hali ya Juu sana tofauti na pale ambapo
wanaporandaranda Mitaani bila kujua na kutambua kuwa mmiliki halisi ni
yupi’aliongeza Bw Livingstone
Pia
alisema kuwa nao wamiliki wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuta sheria za
wataalamu za kuwalinda Mbwa hao kwa kuwapa vyumba maalumu vya kuishi na kisha
kuwafungulia kwa nyakati maalumu hasa nyakati za usiku ambapo hata kwa njia
hiyo itaweza kupunguza kasi ya madhara ya Mbwa kwa binadamu ambayo kila siku
inazidi kukua na kuongezeka kwa Mkoa wa Arusha.
Hataivyo
alisema kuwa mbali na kuweza kuwasaidia Mbwa kwa kuwaVyumba Maalumu vya kuishi
pia wafugaji na wamiliki nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara wanawapa
tiba ya kuweza kuwakinga na magonjwa hasa Chanjo ya kila wiki ambayo nayo
itaweza kuwalinda Mbwa hao dhidi ya Magonjwa yenye madhara hasa kwa Binadamu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment