Na Queen Lema,Arusha
CHAMA CHA KIJAMII CHATOA TAMKO DHIDI YA VIONGOZI WA KIISLAMU
CHAMA cha Kijamii
hapa nchini (CCK)kimeipinga kauli ya Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Shehe
Ponda Isa Ponda ambayo ilikuwa inamtaka Raisi Kikwete atoe amri ya kuwafungulia
waislamu wote walioshikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa ya kufanya
maandamano bila kibali na kufanya uharibifu wa makanisa mbalimbali Jijini Dar
es salaam
Akiongea na waandishi wa habari mapema jana mjini hapa Katibu
mkuu wa chama hicho Bw Renatus Muabhi alisema kuwa kauli hiyo ni kauli ya
uchochezi na uharibifu wa amani hasa kwa mkoa wa Dar es salaam ambapo mpaka sasa madhara mbalimbali
yameshatokea
Alisema kuwa Kiongozi huyo wa dini ya kiislamu hakutoa kauli
nzuri kwani kauli hiyo imechangia sana baadhi ya
waumini wa dini hiyo kupata vichwa na kufanya vurugu huku kama angeweza kutumia
vema nafasi yake aliyonayo katika jamii basi angeweza kurudisha amani hata kwa
kiwango kidogo sana
.
Aliongeza kuwa viongozi hao wa dini wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanatumia vema nafasi yao
katika kuleta amani na badala yake wasitoe matamko mbalimbali ambayo ndiyo
yanayofanya na kusababisha uvunjifu wa amani kwa ajili ya itikadi mbalimbali na
za watu tofautitofauti.
“Hivi karibuni Raisi Kikwete alitoa Tamko ambalo lilikuwa
linaani matukio yalifanywa na baadhi ya watu lakini baada ya muda huyu kiongozi
naye akatoa tamko lake ambalo lilifanya uchochezi mkubwa sana kwa waumini sasa
anapaswa kujua na kutamnbua kuwa anatakiwa kutumia vema nafasi yake katika
jamii kwani kama kiongozi wa dini hakupaswa kutoa tamko la kumuonya Raisi wa
Nchi na badala yake angetumia vema
busara kwa jambo hilo “alisema
Pia alisema kuwa Naye Raisi wa kikwete kuhakikisha kuwa
anawachukulia hatua wote waliohusika na kuamini kuwa yeye ndiye suluhisho la
masuala kama hayo ambayo yanafanya amani ya nchi ya Tanzania kuweza kupotea kwa vyanzo
vidogo vidogo.
Katika hatua nyingine alibainisha kuwa pamoja na kuwa CCK
kinalaani sana matukio kama
hayo lakini nayo Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inawachukulia hatua kali
na za kisheria kwa wale wote ambao
wamehusika kwa namna moja au nyingine katika kuvuruga amani ya Nchi hivi
karibuni kutokana na Matukio ya itikadi za Kidini
Bw Renatus alifafanua kuwa endapo kama Serikali haitaweza
kufanya hivyo basi amani ya Nchi ya Tanzania
itayumba huku hali hiyo ikisababisha sana
kuwepo kwa mdodoro mkubwa wa uchumi hasa kwa watu wa vipato vya chini kwa kuwa
hawataweza kufanya kazi zao sanjari kukithiri kwa vifo ambavyo si vya lazima.
“Kwa mfano kama juzi
kumetokea vurugu kubwa sana hasa maeneo ya Kariakoo ambapo ndipo eneo la Uchumi
mkubwa sana hasa kwa watu wa Dar na
walionekana kuathirika sana ni kina mama pamoja na watoto sasa kama hali nhii
itaendelea hivi ni wazi kuwa tutakuwa tunaruhusu umaskini, lakini kama viongozi
wa Dini watasimama na Serikali itawachukulia hatua basi haya matukio yatakuwa
ni historia kubwa sana kwa jamii “aliongeza bw Renatus
Awali Bw Renatus alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa na
Utii wa sheria pamoja na mamlaka ambazo zipo ndani ya nchi hasa vyombo vya dola
kuwa ni wajibu wao kutambua kuwa jamii inaweza kuwa ni sehemu kubwa sana ya
machafuko ya nchi kwa kufuatafuata mkumbo hasa kutoka kwa viongozi wa Kidini na
Kisiasa kwa malengo ambayo hayajulikani,hivyo wasikubali kutumika kama kuni ili
kuepusha madhara hasa kwa wananchi wa vipato vya chini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment