Na MWANDISHI WETU
HALMASHAURI YA ARUSHA VIJIJINI INAKABILIWA NA UHABA WA
MAPATO
HALMASHAURI ya Arusha Vijijini Mkoani hapa inakabiliwa na
uhaba wa mapato kutokana na baadhi ya watendaji wa halamshauri hiyo kushindwa
kufuatilia kwa undani sana baadhi ya vyanzo vya
mapato hali ambayo kama haitaweza kutatuliwa kwa haraka sana basi itasababisha madhara makubwa hasa
kwenye malengo ya halmashauri hiyo kwenye jamii
Hayo yamebainishwa Wilayani humo na Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo bw Khalifa Idda mapema juzi wakati akiongea katika baraza la
madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baraza hilo pia liliwashirikisha wananchi wa maeneo
mbalimbali ya wilaya hiyo.
Bw Idda alisema kuwa kwa sasa bado kuna upungufu mkubwa sana wa mapato ya
kutosha katika halmashauri hiyo ingawaje ina vyanzo vingi sana vya mapato hali amnbayo inasababisha
kuonekane taa ya hatari hususani katika shuguli za maendeleo ya wananchi wa
wilaya hiyo
Aliongeza kuwa ingawaje wilaya hiyo ina vyanzo vingi sana
vya mapato bado kuna uitaji mkubwa sana wa watendaji wa halamshauri hiyo
kuhakikisha kuwa wanaongeza nguvu zaidi katika kusaka na kubuni aina mpya ya
vyanzo sanjari na kuhakikisha kuwa vyanzo ambavyo vipo vinatoa mapato kwa
mujibu wa sheria na kanuni za Halmashauri hiyo
‘tuna upungufu mkubwa sana wa masuala ya fedha ndani ya
halmashauri yetu nah ii ni kutokana na kuwa
na mapato madogo katika vyanzo vyetu
na hili suala kwa kweli halitupendezi kabisa kwani kama hali itaendelea
hivi ni wazi kuwa hata ,mipango yetu kwa wananchi itakwama sana na
tutasababisha madhara makubwa sana’aliongeza Bw Idda
Pia alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya uhaba wa mapato
kutoka kwenye vyanzo vya kudumu vya Halmashauri hiyo wantarajia kuhakikisha
kuwa kila mkuu wa Idara anatumia vema taaluma yake huku akifuatilia kwa ukaribu
sana vyanzo vyote kwani kama watafanya hivyo
basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana
maendeleo ya mapato
Hataivyo alifafanua kuwa mara baada ya kukaa chini na wakuu
wa idara pamoja na wachumi wa halmashauri hiyo hivi karibuni wataweza kuweka
kipaumbele kikubwa sana na kuhakikisha kuwa wanabuni vyanzo vipya na kuimarisha
vile vya zamani ambapo kama mtendaji wa halmashauri hiyo hataweza kufanya kazi
yake kikamilifu basi watachukuliwa hatua kali na za kisheria.
Katika hatua nyingine madiwani wa baraza hilo
walisema kuwa suala hilo la uhaba wa vyanzo vya
mapato sio suala dogo kabisa kwani linatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka ili
kuweza kunusuru Halmashauri hiyo dhidi ya Majanga mbalimbali ingawaje nao wakuu
wa idara nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawajibika kwa haraka sana.
Madiwani hao walisema kuwa ni aibu kubwa sana kwa
halmashauri hiyo kukosa mapato huku ikiwa na vyanzo vingi sana vya mapato na
aibu hiyo inatakiwa kufutwa na wakuu wa idara hasa Mweka hazina wa Halmashauri
ambapo wanatakiwa kutembea mitaani na kuangali hali ilivyo na kuachana na tabia
ya kudai kuwa halmashauri haina fedha huku vyanzo vingine vikiwa
vinateketea na watendaji wasio
wahaminifu
‘Mweka hazina hapaswi kukaa ofisini na kusubiria taarifa
anatakiwa kutumia taaluma yake vema na kuanza kubuni vyanzo lakini sio hilo
pekee bali anatakiwa pia hata kwenda kwenye vyanzo vya mapato na kama ataweza
kutembelea vyanzo vya mapato kila mara hata watendaji wazembe watajulikana na
wale wanaokula fedha za halmashauri kwa madai kuwa mapato hakuna basi na wao
wataweza kujulikana na hapo tutarudisha vyanzo vyetu jamani tuache kukaa
ofisini na kusubiri kudanganywa na baadhi ya watu “waliongeza madiwani hao
MWISHO
No comments:
Post a Comment