CHAMA cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimetoa onyo kali kwa baadhi ya madiwani wake jijini Arusha walioshiriki katika mchakato wa maandalizi ya uzinduzi wa jiji la Arusha kinyume na msimamo wa chama hicho.
Pia,chama
hicho juzi kiliwaweka kiti moto madiwani hao na kuwahoji kuhusu tuhuma za
kushiriki vikao vya baraza la madiwani la jiji hilo sanjari na kuchukua posho mbalimbali
za vikao hivo ambapo walijieleza na maelezo yao kufikishwa katika ngazi za juu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Arusha, katibu mkuu wa Chadema ,Dk Willbrod Slaa
alisema kuwa iwapo itabainika baadhi ya madiwani hao walijipenyeza na kushiriki
mchakato wa uzinduzi wa jiji hilo pamoja na kuchukua posho za vikao mbalimbali wataadhibiwa
kwa mujibu wa taratibu za chama hicho.
Dk,
Slaa alisema kuwa msimamo wa chama hicho ni kutomtambua meya wa Arusha
,Gaudence Lyimo(ccm)kwa kile alichodai taratibu za kupatikana kwake hazikufuatwa,na
kusisitiza kuwa iwapo madiwani wake wanajipenyeza na kushiriki vikao vya
halmashauri vinavyoongozwa na meya huyo ni utovu wa nidhamu.
‘’kitendo
cha kushiriki vikao vya halimashauri ni kuhalalisha kumtambua meya wa Arusha
sasa sisi msimamo wetu ni kutoshiriki vikao na hata madiwani wanalijua hilo ila
kama wanashiriki kinyemela na kuchukua posho tutapambana nao’’alisema Dk Slaa.
Aidha
dkt Slaa alionya kuwa kitendo cha madiwani wake kushiriki vikao vya
manispaa ni mwanzo mbaya wa kuambikizwa madhambi ya ufisadi yaliyopo
ndani ya manispaa hiyo ukiwemo matumizi mabaya ya fedha za wananchi.
Hata
hivyo mwandishi alipotaka kujua msimamo wa Chadema utaisha lini wakati wananchi
wanaendelea kusota kwa kukosa wawakilishi kwenye kata zao,alisema kuwa diwani
anapaswa kushiriki maendeleo kwenye kata yake na wananchi wake na si kushiriki
vikao vya halmashauri.
Aliongeza kuwa diwani anapaswa kumfuata ofisini mkurugenzi wa jiji na kumweleza matatizo yaliyopo kwenye kata yake bila kushiriki vikao vya baraza la madiwani.
Alipotafutwa
mwenyekiti wa madiwani wa Chadema jijini hapa,Isaya Doita ambaye ni diwani wa
kata ya Ngarenaro alikiri hatua ya wao kuhojiwa na Dk Slaa huku akisema kwamba
kwa sasa hawana la kusema kwa kuwa wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu za
chama.
Hatahivyo,alikiri
wao kushiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji la Arusha hivi karibuni huku akidai
ya kwamba suala la kushiriki na kupokea posho za vikao mbalimbali ni halali
yao.
"sisi tulishiriki katika sherehe hizi za uzinduzi wa jiji kama viongozi wa wananchi na kikao cha kupanga bajeti kilikuwa sio kwenye baraza la madiwani bali tuliitwa katika kikao cha gafla ya madiwani tulivyofika ndo tukaambiwa kuwa ni kikao kwa ajili ya uzinduzi wa jiji na awali mkumbuke tulikaa chini na kuafiki kuwa jiji lizinduliwe mwezi wa kwanza tarehe moja mwakani sasa kwa kuwa watu walikaa na imeamuliwa jiji lizinduliwe tuliamua kushiriki ila sio kikao cha baraza"Doita
"sisi tulishiriki katika sherehe hizi za uzinduzi wa jiji kama viongozi wa wananchi na kikao cha kupanga bajeti kilikuwa sio kwenye baraza la madiwani bali tuliitwa katika kikao cha gafla ya madiwani tulivyofika ndo tukaambiwa kuwa ni kikao kwa ajili ya uzinduzi wa jiji na awali mkumbuke tulikaa chini na kuafiki kuwa jiji lizinduliwe mwezi wa kwanza tarehe moja mwakani sasa kwa kuwa watu walikaa na imeamuliwa jiji lizinduliwe tuliamua kushiriki ila sio kikao cha baraza"Doita
Itakumbukwa
ya kwamba onyo lililotolewa na Dk Slaa limekuja siku chache baada ya madiwani
wa CCM,Tlp na Chadema jijini Arusha kushiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji hilo
kitendo ambacho kimeibua gumzo jijini hapa huku ikikumbukwa ya kwamba madiwani
wa Chadema waliweka msimamo wa kutomtatabua meya wa jiji la Arusha.
Baadhi
ya madiwani wa Chadema walioshiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji hilo hivi karibuni
waliongozwa na diwani wa kata ya
Levolosi,Efatha Nanyaro ambapo alichaguliwa kuwa katibu wa maandalizi ya
chakula cha Rais huku mwenyekiti wake akiwa ni diwani wa kata ya Moshono,Paul
Matyhsen(CCM).
Vilevile
itakumbukwa ya kwamba Chadema kiliwahi kuwatimua madiwani wake watano mwaka
jana ambao ni John Bayo,Ruben Ngowi,Estomi Malah na Rehema Mohamed kwa kosa kuingia
mwafaka wa kumtabua meya wa jiji la Arusha.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment