Saturday, November 24, 2012

VIJANA 200 WA VYUO VIKUU ARUSHA WAPEWA MBINU ZA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA YA MASHARIKI.


Na Queen lema,ARUSHA

VIJANA 200 WA VYUO VIKUU ARUSHA WAPEWA MBINU ZA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA YA MASHARIKI.

Zaidi ya vijana 200 kutoka katika vyuo vikuu vitano mjini Arusha wamefanikiwa kupewa elimu mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia fursa za jumuiya ya Afrika ya mashariki ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya vitu mbalimbali

Akiongea mapema jana  katika mdahalo ambao  umewahusisha vijana kutoka vyuo vikuu vitano vya Arusha mratibu wa mdahalo huo  bw kanani chombara alisema kuwa lengo halisi la kuwapa vijana hao elimu ni kuhakikisha wasomi wote wa mkoa wa Arusha wanazijua na kutambua fursa za soko hilo   

Chombara alisema kuwa wameamua kufanya madahalo huo ambao unahusu fursa mbalimbali za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kuwa asilimia kubwa ya wasomi bado hawajatambua umuhimu wa kutumia fursa zilizopo hasa upande wa ajira na badala yake wana vyuo wa Mkoa wa Arusha wanawaza kupata fursa za kuajiriwa

Alifafanua kuwa hatua hiyo inachangia sana kuweza kupoteza fursa mbalimbali huku kwa upande wa wasomi ambao hawana ajira nao wakiwa wanaongezeka mitaani ingawaje kuna fursa za kutosha

Pia alisema kuwa mara baada ya vijana hao 200  kuweza kupata fursa za kujua na kutambua umuhimu wa fursa za kuwa wasomi kwenye soko hilo na kupitia mdahalo huo ambao utachangia  sana kuongeza amasa kubwa kwa vijana wasomi hivyo kuweza kubuni hata aina mpya ya ajira

‘kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa wanalalamika kuhusu soko hilo lakini bado hawana mcheheto wa kutumia fursa zilizopo kwa kuwa wanasubiri Serikali iweze kuja kuwapa ajira sasa hali hiyo inachangia sana baadhi ya vijana kuweza kuwa wasomi jina huku vijana wa Nchi nyingine wakiwa wanatamia vema fursa ambazo zipo’aliongeza Bw Chombara

Naye mratibu wa shirika la kijerumani (GIZ)bathazar kitundu alisema kuwa shirika hilo limejipanga kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wanatakiwa kujipanga kuanzia wanapokuwa ndani ya Vyuo vyao na kuachana na tabia ya kulalamika.

Bw Kitundu alisema kuwa njia ya kulalamika pekee bado sio suluhisho la kufanikiwa hasa kwa upande wa ajira kwani suluhisho pekee ni kukagua fursa zilizopo na kuweza kuzitumia kulingana  na mahitaji ya Soko hilo ambalo mpaka sasa idadi ya vijana wa Kitanzania wanaotumia ni wachache sana

‘unajua kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa wanalalamika ovyo mitaani lakini wanashidwa kujua kuwa vijana wa n chi nyingine hawana tabia hiyo bali wanaangalia fursa zote sasa hapa kwetu wanataka watafutiwe kupitia elimu  na midahalo kama hii itasaidia vijana wa vyuo vikuu kuweza kufunguka kwa kutafuta fursa ambazo zipo lakini hazitumiwi na wasomi wa vyuo vikuu”aliongeza Bw kitundu.

Alimkalizia kwa kusema kuwa mpango huo wa kufanya midahalo kwa vijana wa vyuo vikuu ili waweze kutumia vema fursa zilizopo ni endelevu ingawaje kwa mkoa wa Arusha mpango huo umeanza na Vyuo vitano ambavyo ni Makumira,Nelson Mandela,Arusha,Tengeru na chuo Kikuu cha IAA.

MWISHO

No comments:

Post a Comment