Watanzania watakiwa kujenga tabia ya kucheki afya zao mara kwa mara
Na Anna Nkinda – Maelezo
…………………………………………
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
ameitaka jamii kujenga mazoea ya kujichunguza afya zao mara kwa mara ili
kuepuka maradhi au vifo visivyo na lazima kwani hivi sasa kuna maradhi
mbalimbali yanayotokana na mazingira na aina ya mtindo wa maisha na
hivyo kurudisha nyuma maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
Mama Kikwete ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ameyasema hayo leo
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji huduma ya afya kwa jamii
ikiwemo uchunguzi wa saratani iliyoandaliwa na Chama cha Madaktari
Wanawake Tanzania (MEWATA) katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
Salam.
Mama Kikwete pia aliitaka jamii
kubadilisha mtazamo juu ya afya ya uzazi na mtoto kuwa inamhusu mama
peke yake bali kila mmoja katika familia anahusika ingawa hapo awali
wanaume walionekana kutengwa na kutowajibika ipasavyo hivyo kusababisha
kuzorota kwa afya ya uzazi na mtoto.
“Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii pamoja na wadau wake hivi sasa wametuanzishia mchakato huu, awali
huduma hii ilijulikana kama afya ya mama na mtoto lakini sasa
inajulikana kama afya ya uzazi na mtoto hii ni kuonesha kwamba kila
mmoja wetu ndani ya familia anawajibika”, alisema Mama Kikwete.
No comments:
Post a Comment