Monday, October 29, 2012

WAMILIKI WA MA MAGARI WATAKIWA KUFUNGA MIKANDA YAO ILI KUEPUSHA AJALI ZA MARA KWA MARA


HUYU NI MMOJA WA WAENDESHA PIKIPIKI JIJINI DAR ES SAALAM AKIONESHA MANJONJO YAKE LAKINI KWA SASA NDANI YA MJI WA ARUSHA PIKIPIKI ZIMEKUWA SABABU YA AJALI KUBWA SANA 


WAMILIKI wa magari ya abiria mkoani arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa
magari yote yanakuwa na mikanda  na kila dereva kuhakikisha kabla ya
kuondoka kituoni  kila  abiria  amefunga mkanda wake ili kusaidia
kupunguza vifo vinavyotokana na   ajali zinazotokea mara kwa mara.

Hayo yalisemwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kwa mkoa huu
Marison Mwakyoma  alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusiana na
uchunguzi waliobani kutokana na magari ambayo hayana mikanda ya
abiria.

Alisema kuwa wakati wakiendelea katika zoezi  la wiki ya nenda kwa
usalama barabarani wamegundua kuwa magari mengi hayana mikanda ya
abiria na hata yaliyonayo ni mibovu hali ambayo inafanya kuzidi
kuongezeka kwa vifo mara panapotokea ajali.

Alieleza kuwa baadhi ya magari yenye mikanda hiyo  abiria wao
wanakataa kuifunga kwa madai kuwa ni michafu  hivyo kuwataka wamiliki
wa magari wenye mikanda michafu kuibadilisha mapema iwezekanavyo kwa
kuwa yeyote atakayebaini  bila kufunga mikanda hiyo sheria
itachukuliawa dhidi yake.

“kwa sasa tumeshaweka sheria kwa wale wote watakaokutwa bila kufunga
mkanda wanachukuliwa hatua ya kupigwa faini hivyo nawasisitizieni sana
wamiliki na madereva wa magari muwe makini kuhakikisha kuwa kila
abiria amefunga mkanda wake na pia kama mikanda yenu ni mibovu
badilisheni kwa haraka”aliongeza Mwakyoma.

Pia aliwasihi abiria nao kuwa na desturi ya kufunga mkanda  na wawe na
msimamo wa kutopanda gari ambalo halina mikanda na wasikubali
kulazimishwa endapo hakuna mikanda hiyo.

Aidha aliwataka wamiliki wa mabasi kuhakikisha kuwa kabla
hawaajaajiri madereva wao wahakikishe kuwa wana leseni kwa kuwa
wamegundua kuwa baadhi ya madereva hawana leseni huku wengine wakiwa
na leseni za kughushi  hali inayowapelekea kukamatwa na kulipa faini.

Aliongeza kuwa nao madereva wanaopandisha nauli mara ifikapo mida ya
jioni watachukuliwa hatua kali kwa kuwa wanakiuka sheria na taratibu
zilizowekwa bila kujua kuwa wanaoumizwa ni wananchi hasa wenye vipato
vya chini.

Hata hivyo aliwataka madereva kupeleka magari yao kituoni ili yaweze
kukaguliwa  ili yawe salama yaweze kupunguza ajali barabarani.
mwisho




No comments:

Post a Comment