Tuesday, November 20, 2012

RAISI KIKWETE AZINDUA MKAKATI WA PILI WA NCHI WANACHAMA WA SADC

DKT JAKAYA KIKWETE AKIWASALAMIA WANANCHI,HAWAPO PICHANI HIVI KARIBUNI MKOANI ARUSHA,PICHA NA MAKTABA


RAISI KIKWETE AZINDUA MKAKATI WA PILI WA NCHI WANACHAMA WA SADC

WAANDISHI WETU,ARUSHA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi mkakati wa pili wa chombo cha nchi wanachama wa SADC ambapo chombo hicho kitashugulikia masuala mbalimbali kama vile Siasa,Ulinzi na Usalama (SIPO)

Akiongea na Waandishi wa habari mapema jana mara baada ya kuzindua chombo hicho Raisi Kikwete alisema kuwa chombo hicho kitasaidia sana kuweza kufanya mabadiliko ya hali ya juu sana hasa kwa nchi husika.

Alisema kuwa mkakati huo ambao ni mpya utasaidia sana kufanya mabadiliko makubwa sana hasa katika nyanja za Siasa,ulinzi, na usalama ambapo pia matarajio ya chombo hicho ni kuona kuwa mabadiliko yanachangia hata maendeleo

Alifafanua kuwa,kwa Nchi mbalimbali za SADC ambazo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vita mkakati huo utaweza kuwasaidia  hata katika  kutafuta muafaka na kuepukana na vita ambavyo  ni chanzo kikuuu cha vifo ambavyo havina hatia

‘tukiangalia suala la nchi zenye Vita hasa Demokrasia ya Kongo Mkakati huu utachangia sana kuweza kuleta Muafaka kwani tutahakikisha kuwa tunakaa meza moja na kumaliza vita kwa njia ya usuluhishi na hapo sasa ndio maana halisi ya chombo hiki’aliongeza Dkt Kikwete

Katika hatua nyingine alisema kuwa kupitia kweenye Chombo hicho cha kinachohusika na masuala ya Ulinzi,Usalama, na Siasa pia wataweza kuyuuunda Majeshi ya pamoja la kulinda amani katika nchi zenye vita ikiwemo Kongo.

Awali katibu mkuu wa Nchi wanachama wa SADC dr Tomaz Augusto alisema kuwa kupitia chombo na mkakati huo utasadia kuimarisha umoja ,maendeleo na mshikamano kwa nchi wanachama hali ambayo nayo itachangia sana kuweza kupunguza umaskini.

Dr  Tomaz  aliongeza kuwa mbali na hayo pia utaweza kujikita katika masuala mbalimbali hasa ya Uchumi ambapo chombo hicho kitaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanasiasa huku lengo likiwa ni kulinda amani

Katika  hatua aliwataka wanachama wa Nchi za SADC kuimarisha uhusiano ikiwa ni pamoja na kuuungana na kuwa kitu kimoja ili kuweza kufikia malengo mbalimbali ambayo wamejiwekea hasa katika nyanja ya kupambana na umaskini,pamoja na ukosefu wa elimu hali ambayo inasababisha vita mara kwa mara.

MWISHO

No comments:

Post a Comment