MBOWE -ACHENI PROPAGANDA FEKI
MWENYEKITI
wa Chadema,Freeman Mbowe amesema watu wanaoeneza propaganda na kupanda mbegu
chafu kwa kudai kuwa Chadema ni chama cha wachaga wamepoteza dira na kuhishiwa
na hoja.
Mbowe
aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa Manyara kwenye
uwanja wa Kwaraa mjini Babati katika ziara ya Chadema ya operesheni vuguvugu la
mabadiliko (M4C) mkoani humo.
Alisema
wanaoeneza fikra hizo potofu zisizo na mashiko wameishiwa na hoja na aliongeza
kuwa Chadema hakifungamani na kabila wala dini yoyote ile kwani viongozi wake
ni wametokana na dini tofauti na makabila mbalimbali.
Alisema
Makamu wake upande wa bara Said Arfi ametokea Mpanda na wa upande wa Zanzibar ametokea Wete
Pemba na Katibu Mkuu Dk Wilbroad Slaa ametokea Karatu na Naibu Katibu Mkuu
Zitto Kabwe ametokea Kigoma.
“Kwa
vile mimi ni mchaga wanasema Chadema ni chama cha wachaga,mbona Chama
kinachoitwa mapinduzi sijui walipindua nini,Mwenyekiti wake ni mkwere lakini
hakiitwi chama cha wakwere,” alisema Mbowe.
Alisema
hata Wenyeviti wa TLP na NCCR-Mageuzi ni wachaga lakini vyama hivyo havisemwi
kuwa ni vya wachaga ila Chadema kwa vile jamii inawaunga mkono na watu wamepata
mwamko kuwafuata wanadai ni chama cha wachaga.
Aliwataka
wakazi wa mkoa wa Manyara wajiandae kwa ajili ya mabadiliko kwa kuitoa CCM
madarakani na kuiweka Chadema kwa njia ya kura mwaka 2015 na wajitokeze kwa
wingi wakati wa kujiandikisha utakapofika.
Alisema
mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa CCM ndiyo sababu wanashiriki
kutetea na kutoa hamasa kwa watanzania wote bila kubagua eneo alilochaguliwa.
“Wabunge
wa Chadema ni watu makini ndiyo sababu leo Halima Mdee mmemuona hapa
Manyara,japokuwa yeye ni mbunge wa Kawe na Pauline Gekul naye hata nje ya nchi
huwa nakwenda naye,” alisema Mbowe.
Naye,Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Manyara (Chadema) Pauline Gekul alisema CCM imekosa dira
na mwelekeo katika mkoa huo hivyo wanasubiri kwa hamu kufanyika kwa uchaguzi
mkuu ili waiondoe madarakani.
“Wana
wa Manyara wamechoka na CCM hivyo Kamanda Mbowe wana kuhakikishia kwa kusema
CCM kwisha,kwisha,kwisha kabisa na jibu ni mwaka 2015 pale ambapo watakapoitoa
madarakani kwa njia ya kura,” alisema Gekul.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment