Na
Queen Lema, Arusha
TAASISI
ZA FEDHA ZASHAURIWA KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI
TAASISI
za Fedha zimeshauriwa kuhakikisha kuwa wanapeleka huduma zao hata Vijijini kwa
kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Vijijini hawana uelewa wa kutosha juu ya
matumizi ya Taasisi hizo za fedha hali ambayo nayo inachangia kukithiri kwa
changamoto mbalimbali zikiwemo za matumizi mabaya ya fedha na mali
Kauli
hiyo imetolewa mjini hapa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Trasias Kagenzi
wakati alipokuwa akiongea na Walimu mbalimbali ambao ni wadau wa Benki ya NMB
katika Siku ya Mwalimu iliyoazimishwa na Benki hiyo.
Kagenzi
alisema kuwa kwa sasa Taasisi nyingi sana za
fedha zimejikita zaidi kwenye maeneo ya Mijini huku kwa upande wa Vijijini
wakiwa wamesahulika ingawaje kijijini ndiko kwenye fursa nyingi sana za Fedha ambazo zimesahulika sana
hali ambayo nayo inachangia sana
Umaskini.
Aliongeza
kuwa Taasisi hizo za Fedha zinatakiwa kubadilisha na kuimarisha mifumo zaidi
hasa Vijijini ambapo kuna fursa nyingi lakini hazitambuliki kutokana na
wananchi kushindwa kujimudu kimaisha lakini kama Taasisi za Fedha zingejikita
zaidi basi hata uchumi wa vijiji pamoja na Mikoa ingeweza kuimarika sana na kufanya hata kiwango cha uzalishaji kuwa kikubwa sana.
“kwa
sasa hasa ndani ya Mkoa wa Arusha Mjini unakuta kila mahali ni benki lakini
ukija vijijini hakuna hata benki ya kugeresha maisha sasa hawa Wamiliki wa
Mabenki na Taasisi za Fedha wanasahau kuwa ambaye anaweza kujikwamua zaidi
kiuchumi ni mtu wa Kijijini kwa kuwa ndani ya Vijiji kuna fursa Nyingi sana
hasa za Kilimo, na Ufugaji hivyo basi napenda kuwakumbusha kuwa mnatakiwa
kuwakumbuka hata wananchi wa Vijijini hata kwa kuwapa elimu ya kumiliki
fedha”aliongeza Bw Kagenzi
Pia
alisema kuwa mbali na Mabenki hayo kuweza kuwekeza zaidi Vijijini lakini nao
wafanyakazi hasa ambao ni waajiriwa wa Serikali wanatakiwa kuijiendeleza kwa
kuhakikisha kuwa wanatumia fursa mbalimbali za Mabenki hasa NMB kwa kuhakikisha
kuwa wanakopa na kisha kufanyia Mikopo yao
kazi za maendeleo kwa manufaa ya Jamii zao.
Awali
Meneja wa Benki hiyo kwa kanda ya Kaskazini bi Vicky Bishubo alisema lengo
halisi la kuwakutanisha walimu wa shule mbalimbali ni kuweza kuwapa elimu
mbalimbali ikiwemo huduma zinazotolewa na Benki hiyo hali ambayo itawafanya
wadau hao kuweza kufikia malengo yao
mbalinbali ya Kimaisha.
“kama
tunavyojua ni kuwa benki yetu mpaka sasa imeshatoa mikopo mingi sana kwa walimu
na walimu ni wadau wetu wa muhimu sana sasa tunapowakutanisha hivi katika siku
ya Mwalimu ndani ya benki hii tunaweza kuwaongezea uwezo wa kutumia fursa
zilizopo ambazo kama nazo watazitumia vema basi wataweza kufikia malengo yao
mbalimbali’aliongeza Bi Vicky
MWISHO
No comments:
Post a Comment