MULTICHOICE YAPUNGUZA MALIPO YA MWEZI KWA 10%
Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.
Peter Fauel, akitangaza Punguzo la Asilimia Kumi ya Malipo ya mwezi kwa
wateja wa Televisheni kwa Vipindi vya DStv likaloanza hapo kesho,
ambapo amesema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma za
Matangazo ya Televisheni ya kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia amesema
Offer hiyo ya Punguzo la bei ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha fadhila
kwa wateja wake kuelekea katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu za
mwisho wa mwaka. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice
Barbara Kambogi na Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Furaha
Samalu.
Meneja Masoko wa Multichoice wa Kampuni
hiyo Bi. Furaha Samalu akitoa ufafanuzi kuwa katika kipindi hiki cha
kuelekea matumizi ya mfumo wa Digitali DStv kwa kuwajali wateja wake
imepunguza gharama za kuunganishwa ambapo sasa ni kwa shilingi za
Kitanzania 169,000 unaweza kusheherekea msimu wa sikukuu na DStv.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice Barbara
Kambogi (wa pili kushoto) akiwahakikishia wateja wa DStv kuwa sasa
kampuni hiyo imezidi kuboresha huduma zenye viwango vya hali ya juu na
kuwataka wazazi kutumia fursa hii ya punguzo la bei ya kuunganishwa ili
watoto wao waweze kushuhudia vipindi mbali mbali vya kuelimisha na
kuburudisha ikiwemo filamu kali, katuni maridadi, michezo mbalimbali
katika kipindi hiki cha likizo kwa watoto wao na kuwa huu ndio sasa muda
muafaka kwa kujipatia DStv.
Meneja Mauzo wa DStv Tanzania Bw.
Salum Salum akifafanua kuwa Multichoice imepanua wigo wa kutoa huduma
kwa wateja ambapo sasa wanamawakala 200 nchini na kuwataka wanapokwenda
kulipia Ving'amuzi vyao ni lazima wahakikishe vimewashwa ili
kurahisisha kufanyika kwa huduma hiyo pia amesema wateja wa DStv
wanaweza kufanya malipo ya huduma hiyo kupitia simu za mkononi na
ukizingatia kampuni hiyo imeongeza maeneo ya kutoa huduma ikiwemo Uchumi
Super Market, Kariakoo na Mlimani City kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Kampuni ya MultiChoice imetangaza punguzo
la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa wateja wa televisheni kwa vipindi
vya DStv litakaloanza kesho Novemba 15, 2012.
Meneja Mkuu wa MultiChoice Tanzania,
Peter Fauel alisema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma
za matangazo ya televisheni ya kituo hicho kwa gaharama nafuu.
Fauel alisema kwa wateja watakaokuwa
wamelipia tayari huduma hiyo ndani ya mwezi huu,
wataendelea kutumia
hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha, kisha wataanza na bei mpya ya
punguzo kuanzia mwezi unaofuata ila wahakikishe huduma yao kutokatika.
"Tumedhamiria kuwapunguzia wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida," alisema Fauel.
Meneja mkuu huyo alisema, kuwa kama
kawaida yao huwapa wateja wao unafuu wa bei kulingana na kipato chao,
hivyo punguzo hilo litawanufaisha kwa kiwango kikubwa ili kila mmoja
afaidi burudani.
Alisisitiza kuwa DStv itaendelea
kuwapatia Watanzania na Waafrika kwa ujumla vipindi vyenye ubora kwa
vile wamewekeza katika vipindi vipya.
Kwa wateja watakaonufaika na ofa hii, wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa 150,000 kwa mwaka!
Fauel akaongeza kwamba “Tunawaahidi
wateja wetu huduma bora na kwamba kwetu mteja ni mfalme. Mtandao wetu wa
usambazaji unazidi kupanuka na sasa tupo kila mkoa wa nchi. Pia
tunafurahi kwamba sasa tuna ofisi zetu Kariakoo na supermarket ya Uchumi
iliyopo barabara ya Pugu. Hii itawarahisishia wateja wetu kupata bidhaa
na huduma zetu kwa haraka zaidi.
No comments:
Post a Comment