NA MWANDISHI WETU,ARUSHA
IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi mbalimbali ambao
wanahisiwa kukabiliwa na nguvu za giza
hawana nguvu hizo na badala yake wanafunzi hao wanakabiliwa na hali ya uoga
hasa nyakati za mithiani,hali ambayo inasababishwa na mazingira ya majumbani
mwao pamoja na shule zao
Wakati wa Mithiani asilimia kubwa ya wanafunzi huwa
wanaanguka na kushindwa kufanya mithiani lakini sio nguvu za giza
bali ni uoga wa mithiani na msongamano mkubwa sana wa mawazo (STRESS)
Hayo yamebainishwa wiki iliyopita na Bw
Japhet Mwanangombe ambaye ni mratibu wa
shirika lan Roots and Shoots la jijini hapa wakati akiongea katikia
kongamano la wanafunzi wa shule mbalimbali mjini hapa ni wanamazingira kwa
kanda ya kaskazini
Bw Japhet alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi
wanasumbuliwa na hali ya uoga mkubwa sana hasa
nyakati za mithiani ya Mwisho wa Mwaka pamoja na mithiani ya Kitaifa huku
wazazi, walezi, na walimu wakijua kuwa ni nguvu za giza
hali ambayo inafanya hata baadhi ya maendeleo ya Taaluma kushuka sana hasa kwenye baadhi ya
shule.
Aliongeza kuwa wanafunzi wengi huwa wanafikiria zaidi
matokeo ya mithiani au hali duni za maisha yao
majumbani mwao bila kujua na kutambua kuwa mawazo kama hayo ndiyo yanayochangia
kupoteza fahamu huku watu wengine wakihisi kuwa wanakabiliwa na changamoto ya
nguvu za giza
ndani ya shule zao
‘kwa kweli uchunguzi ambao tumeufanya kwa baadhi ya shule
hasa za kanda hii ya kaskazini ambazo zinakabiliwa na changamoto kama hiyo
tumebaini kuwa hakuna hata chembe ya nguvu za giza ila kwa kuwa wazazi na
walimu wamejiwekea utaratibu wa kudai ni nguvu za giza na watoto wanaamini
hivyo ila sio kweli wengi wanaogopa mithiani na matokeo ya mithiani,pamoja na
hali duni za majumbani mwao’aliongeza
Katika hatua nyingine alisema kuwa ili hali hiyo iweze
kupotea kwenye baadhi ya shule hasa kwa kanda ya kaskazini wazazi pamoja na
walimu wanatakiwa kuhakikisha kuwa kwanza wanawajengea uwezo wanafunzi wa kuwa
wajasiri wa kukabiliana na mithiani pamoja na hali duni za maisha ambapo kama
watafanya hivyo basi watachangia sana wanafunzi kuacha kuanguka anguka ovyo.
Alisistiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwapa moyo watoto wao
hasa nyakati hizo za mithiani na kuacha tabia ya kuwapa vitisho ambavyo ndivyo
vinachangia baadhi ya shule kukumbwa na na kashfa ya kuangukaanguka huku pia
hali hiyo nayo ikichangia matokeo mabaya sana
hasa kwenye mithiani ya Kitaifa
‘wakati wa mithiani wapo watoto ambao wana uwezo wa kufanya
vizuri kabisa lakini wanashindwa kufanya vizuri kwa kuwa wazazi na walezi wao
wanawapa vitisho vikubwa sasa hapa unakuta kama mtoto hajaanguka na mawazo,
basi anafanya vibaya hii ni hatari sana
kwa maendeleo ya taaluma hapa nchini”aliongeza
Awali wanafunzi wa
klabu hiyo walisema kuwa idadi ya wanafunzia ambao wanadondoka hasa nyakati za
mithiani(EXAMINITIONAL FEVER) inaongezeka siku hadi siku lakini shule za
Msingi,Sekondari, na Vyuo vinatakiwa kuwa na kitengo maalumu cha kuwapa
wanafunzi ushauri ili kuweza kuwajenga zaidi tofauti na sasa ambapo baadhi ya
wakuu wa shule na walimu wanatoa vitisho kwenye mithiani ya Kitaifa
Mwisho
No comments:
Post a Comment