Na Queen Lema,ARUSHA
ZAIDI ya wakazi 6000 kutoka katika kata ya daraja mbili
mkoani hapa wanatarajiwa kufikiwa na elimu ya mazingira ingawaje kwa sasa bado
mitaa mbalmbali ya Kata hiyo inaongoza kwa uchafu na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vikiwemo
vyanzo vya maji hali ambayo inachangia mlipuko wa magonjwa na ukame
Hayo yameelezwa jana na mtatibu wa shirika la Initiative for
youth(INFOY) bw Laurent Sabuni wakati akiongea na wananchi wa mitaa mbalimbali
ya Kata hiyo ambayo bado inakabiliwa na tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira
kutokana na uhaba wa elimu ya utunzaji wa mazingira
Bw Laurent alisema kuwa wananchi hao watafanikiwa kupatiwa elimu
kuanzia sasa ambapo elimu hiyo italenga kufanya kata hiyo kuwa katika hali ya
usafi kwani kwa sasa hali ya usafi katika kata hiyo ni mbaya sana
hususani kwa nyakati kama hizi ambazo Mvua
zinatarajiwa kuanza kwa wakati wowote ule.
Alisema kuwa wamelazimika kutoa elimu hiyo ili kufanya kata
hiyo na mitaa yake kuwa na usafi wa kutosha ilin kuepusha madhara mbalimbali
ambayo yanajitokeza kutokana na uchafu uliokithiri pembezoni mwa barabara na
hata katika vyanzo mbalimbali vya maji hususani Mito ambayo inazunguka kata hiyo
“tumelezimika kushirikiana na wenzetu wa Foundation for
Civil Society kuweza kuokoa afya za watu hawa 6000 ambao miongoni mwao wapo
watoto kwani hali ya usafi bado ni ndogo
sana ingawaje kwa sasa Jiji linahimiza kufanya hivyo sasa kwa hiyo hawa
watakaopata elimu hii tunatarajia kabisa wataweza kufanya mabadiliko makubwa
sana”aliongeza Bw Laurent
Pia alisema kuwa ili kuhakikisha zoezi hilo
la kuokoa maisha ya watu wa kata hiyo ya daraja mbili linafanikiwa kwa kiwango
kikubwa pia wamefanikiwa kujiwekea taratibu mbalimbali ambazo zitatumika
kulinda mazingira mbalimbali ya Kata hiyo ambapo taratibu hizo zitawafanya
wachafuzi wa mazingira kuepukana na tabia hiyo kwa kuhofia kufikishwa
mahakamani na kutozwa faini kubwa sana
Alibainisha kuwa nazo kata nyingine zinatakiwa kuhakikisha
kuwa zinakuwa na sheria kali sana hasa kwa wachafuzi wa mazingira kwani bado
jamii inakabiliwa na watu hao kwa kuwa
wanafikiri kuwa sheria hazipo na kama zipo hazitekelezwi huku hali ikisababisha
baadhi ya mitaa ya Jiji la Arusha kukithiri kwa kiwango kikubwa sana cha uchafu
“Mitaa kupitia Serikali zake zinatakiwa kuhakikisha kuwa
sheria mbalimbali za utunzaji wa mazingira zinafutwa lakini kama
sheria zitakuwa zinawekwa maofisini pekee na kushindwa kufafanuiliwa kwa
wananchi huku hali ikisababisha baadhi ya watu kutumia fursa hiyo kuchafua
mazingira ovyo na kufanya hata jitiada mbalimbali za wadau wa mazingira
kushindwa kutekelezwa kwa wakati”alisema Bw Laurent
MWISHO
No comments:
Post a Comment