Thursday, October 11, 2012

Milioni 48/= zapatikana kuchangia shule ya watoto yatima



Na..John Ngunge .....Arusha

JUMLA ya Sh. milioni 48 zimepatikana katika harambee ya kuchangia
shule ya watoto yatima ya Peace House, iliyopo Kisongo nje kidogo ya
jiji la Arusha inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kati.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo iliyoambatana na mahafali ya pili
ya kidato cha nne,  mgeni rasmi Askofu wa Dayosisi ya Kati,   Dk.
Thomas Laizer, alisema watoto yatima ni sehemu ya jamii, hivyo ni
vyema kama jamii ikabadili mtizamo wao na kuwapatia haki sawa
iliwaweze kufikia malengo yao kama ilivyo kwa watoto wengine.

Alisema jamii imekuwa ikiwatenga watoto yatima hasa ndugu wa yatima
hao hali ambayo inawafanya wakose mahitaji ya msingi kama elimu.
Aidha amesema watoto yatima wanahitaji mahitaji  muhimu kama walivyo
watoto wengine na pindi wanapopata nafasi ya kujiendeleza kielimu
daima huwa wanafanya vizuri.

Pia aliwahimiza Watanzania kuendelea kuwasaidia yatima bila kusubiri
wafadhili kutoka nje kwa kuwa vitabu vitakatifu vya dini vinahimiza
kuwasaidia watoto hao ambao wengi wao wamejaa sononeko la kuondokewa
na wazazi.

Mkuu wa shule hiyo, Christopher Mushi, alimshukuru Askofu Laizer na
wadau wote waliochangia harambee hiyo kwa kuwa wamesaidia kwa kiasi
kikubwa kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili kwa sasa baada ya
kujitoa kwa wafadhili wa shule hiyo walijitioa kufadhili.

MWISHO

No comments:

Post a Comment