Naibu Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akifungua mkutano 22 wa mwaka wanachama wa mfuko wa pensheni wa (PPF)
………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Mifuko ya jamii hapa nchini imetakiwa kufanya utafiti wa
kina ili kubaini wanachama wapya kutoka kwenye sekta isiyo rasmi kwani
sekta hiyo imekuwa ikikuwa kwa kasi na kuajiri watu wengi hivyo wajikite
kutafuta wateja wapya kwenye sekta hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa fedha Mh.Saada Mkuya
Salum wakati akifungua mkutano 22 wa mwaka wanachama wa mfuko wa pesheni
wa (PPF)na wadau mbali mbali wa mifuko ya hifadhi za jamii kutoka nchi
za Sadc.
Mh.Mkuya aliwataka PPF na wadau
wengine kuisidia serikali kukuza uchumi kwa kuweka misingi endelevu ya
uendeshaji wa huduma muhimu za hifadhi ya jamii hapa nc hini katika
mazingira haya ya utandawazi na kuwaasa viongozi wa mifuko ya hifadhi za
jamii kuhakisha mifuko yao inaongeza mapato yatokanayo na uwekezaji wa
miradi mbali mbali sanjari na usajili wa wanachama wapya.
Mh.Mkuya pamoja na kuupongeza
mfuko wa PPF kwa jitihada zao za kuhakikisha maendeleo ya kweli
yanapaitikana hapa nchini zikiwemo ujenzi wa nyumba za bei nafuu pamoja
na utoaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo na viwanda na kuwataka
kuendelea kuwekeza zaidi hususani katika sekta za maendeleo ya kijamii
wanachama wake waendelee kufaidika.
“Naomba kutoa wito kwa mifuko ya
hifadhi ya jamii kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta za maendeleo ya
kijamii ili wanachama wanufaike na zoezi hilo liende sambamba na mifuko
hiyo ya hifadhi ya jamii kutoa elimu kwa wanachama juu ya vipi
wanavyofaidika kutokana na uwekezaji huo”alisema Saada.
Aidha mwenyekiti wa bodi ya
wadhamini wa PPF Dkt. Adolfu Faustine Mkenda alisema kuwa mfuko wa PPF
unaendelea kufanya vizuri kwa thamani ya mifuko kuongezeka kufikia
shilingi bilioni 894.52 kutoka shilingi 722.47 bilioni mwishoni mwa
mwaka 2010 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 23.8% ambapo hadi
kufikia mwezi wa sita mwaka huu thamani ya mfuko iliongezeka na kufikia
984.99 bilioni.
Mkenda alisema kuwa idadi ya
wanachama imeendelea kuongezeka hadi kufikia wanachama 180,049 mwishoni
mwa mwaka 2011 ikilinganishwa na wanachama 160, 068 waliokuwepo mwishoni
mwaka 2010 na hadi mwezi juni mwaka huu wanachama wameendelea
kuongezeka zaidi na kufikia 195,347.
Pia aliongeza kuwa michango ya
wanachama iliyokusanywa kwenye mifuko hadi kufikia mwezi wa sita mwaka
huu 111.44 bilion zimekusanywa ambapo lengo lilikuwa ni kukusanya
shilingi 108 bilion kwa kipindi cha miezi sita ambayo ni sawa na 103% ya
makisio ambapo mfuko umeendelea na uwekezaji katika vitega uchumi na
jumla ya shilingi 837 bilioni ziliwekezwa kufikia mwishoni mwa mwaka
2011 ukilinganisha na mwaka 2010 na hivyo kuvuka lengo la mapato yao.
Nae mkurugenzi wa PPF hapa
nchini William Erio alisema kuwa shirika linakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo ya kubadilika kwa riba katika amana za uwekezaji,kiwango
kikubwa cha mfumuko wa bei, ufinyu wa wigo katika uwekezaji na zingine
ni uwasilishwaji wa fomu kutoka kwa waajiri au kutowasilisha,
ucheleweshaji wa michango, hivyo shirika limeamua kukabiliana kikamilifu
na changamoto hizo ili kuleta tija na mafanikio kwa wanachama wao.
No comments:
Post a Comment