Na Queen Lema,Meru
VIONGOZI mbalimbali wa siasa, wazazi pamoja na walezi
wameombwa kuwekeza nguvu zao zaidi katika elimu na kuachana na tabia ya
kuwekeza zaidi katika anasa, na sherehe mbalimbali huku sekta hiyo
ikikabiliwa na changamoto kubwa sana za
uhaba wa vyumba vya madarasa, pamoja na uhaba wa mabweni huku hivyo vikiwa ni
vikwazo vya kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu
Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni Wilayani Meru na Mjumbe wa
kamati ya siasa wilaya ya Meru,Bw William Sarakikya alipokuwa mgeni rasmi
katika harambee ya kuongeza vyumba vya madarasa kwa shule ya Sekondari ya
Unambwe .
Alisema kuwa Changamoto ambazo zipo kwenye shule za
Sekondari ndani ya Wilaya hiyo ni nyingi sana ingawaje wilaya hiyo ni moja ya
wilaya yenye wadau wengi sana wakiwemo wana siasa ambao mara kwa mara
wanachangia Sherehe mbalimbali tena kwa kutambiana sana kwa kuwa na fedha
nyingi sana.
Aliongeza kuwa matambo ambayo yanatumika na wadau hao
mbalimbali wakiwemo wanasiasan yanatakiwa kutumika ndani ya shule mbalimbali kwa kuhakikisha kuwa shule
hizo zinakuwa na maitaji muhimu sana kwani Elimu ni Urithi ambao ni wa kudumu
tofauti na sherehe pamoja na anasa za dunia.
“unapochangia sherehe unakula unasahau lakini kama
tutaoneshana ubabe wetu hasa sisi wanasiasa kwa kushika shule ambazo
zinatuznguka na kuanza rasmi Harambee basi tutachangia kwa kiwango maendeleo ya
shule hasa kwa kipindi hiki ambacho kina umuhimu mkubwa sana wa kuwa na mabweni
hasa upande wa wanafunzi wa kike”aliongeza
Pia alisema kuwa nao wazazi hasa wa Wilaya hiyo ya Meru
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawapa watoto fursa ya kupata elimu bora kwa
kuhakikisha asilimia kubwa ya wanafunzi wanakaa Bweni ili kuweza waweze kupata
muda wa ziada wa kujisomea mashuleni tofauti na wanapokuwa majumbani mwao.
“Nawasihi sana wazazi wenzangu hakikisheni hii wilaya
inakuwa ni moja ya wilaya yenye mabweni mengi sana ili hawa watoto wetu waweze
kupata muda wa ziada wa kujisomea tofauti n pale ambapo wanapokaa majumbani
mambo yanakuwa ni mengi sana hivyo
kusababisha wanafunzi wetu kukosa hata muda wa kujisomea huku hali hiyo
ikisababisha mdondoko wa elimu”aliongeza Bw Sarakikya.
Awali,Wanafunzi wa shule hiyo ya Unambwe walisema kuwa ili
waweze kufanya mithiani yao
ya mwisho vema ni lazima changamoto za msingi ziweze kutatuliwa kwani wapo
wanafunzi ambao wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika masomo lakini
wanakwamishwa na changamoto hizo.
Walitaja Changamoto hizo ambazo ni kikwazo pekee cha
kuwafanya washindwe kufikia viwango bora vya kufaulu kuwa ni pamoja na
changamoto ya uhaba wa madarasa, uhaba wa walimu,uhaba wa vifaa kwa ajili ya
maabara hali ambayo ni chanzo cha ongezeko kubwa sana la Mbumbumbu ndani ya
Taifa la Leo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment