MAJIRA YA KILIMO HASA UPANDAJI NA UVUNAJI ASILIMIA KUBWA YA
WAKRISTO WANAKWEPA MAKANISA YAO.
Na Bety Alex, MERU
MAKANISA ya pembezoni mwa miji na ndani ya Vijiji mbalimbali
kwa mkoa wa Arusha yanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na waumini wachache
sana hasa
katika majira ya Upandaji na Uvunaji hali ambayo inasababisha Mipango
mbalimbali ya makanisa hayo kukwamaa
Asilimia kubwa ya wakristo hasa maeneo ya Vijijini
wanashindwa kuhudhuria nyumba za ibada kwa misimu kama ya kilimo huku hali hiyo
ikisababisha baadhi yao
kushindwa kusonga mbele zaidi katika masuala ya kiroho na kukwamisha shuguli
mbalimbali za kanisa.
Changamoto hiyo imeeelezwa na Mchungaji William Ayo wa
kanisa la AMEC,usharika wa kileleni Kikatiti Wilayani Meru mkoani hapa wakati
akizungumza katika Harambee ya ujenzi wa kanisa
hilo
iliyofanyika kanisa hapo wiki iliyopita.
Alisema kuwa makanisa hayo ya Vijijini tena yaliyo mengi sana yanakosa hata waumini kwa nyakati kama hizo ambapo
asilimia kubwa sana
ya wanaelekea kwenye nyakati za kulima na kufuga huku Mungu naye akiwekwa kando
mpaka mazao yatakapovunwa
Alibainisha kuwa hali hiyo ni hatari sana kwa maisha ya
kiroho kwani muda na nyakati kama hizo shetani anatumia mwanya huo kuchukua
mali zake na kusababisha madhara makubwa sana kwa jamii wakati kwa wale ambao
wanaamini kwa majira yote wanaweza kuwa huru zaidi.
“asilimia kubwa sana ya watu wanaumiza akili zao na mawazo
mengi sana kuwaza juu ya vitu vya dunia na kuacha kumuwaza zaidi Mungu kwani
wakati wa kilimo wengi wanawaza kupatra mazao mengi zaidi kuliko kumuwaza Mungu
aliyejuu na hii inachangia sana hata makanisa mengi sana kuweza kushinda
kutekeleza mipango yake mbalimbali ambayo wamejikea kwa kuwa hakuna watu
wanakuja katika nyumba za ibada kwa misimu pekee”aliongeza
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa nayo makanisa ya
Vijijini yanatakiwa kuacha kukata tamaa juu ya kuwaombea watu wake ambao
wanawaza na kutumia zaidi muda wao katika kutafakari majira ya Mwaka na badala
yake wahakikishe kuwa wanawaombea na kwenda kuwaleta kwani wakiwa nje ya kundi
kwa ajili ya Kilimo wanakuwa na muda mzuri wa kumtumikia zaidi Shetani kuliko
Mungu
Hataivyo aliongeza kuwa nao wadau mbalimbali wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanajijengea hata tabia ya kuchangia makanisa ya Vijijini
kwani asilimia kubwa ya watu wanachangia zaidi makanisa ambayo yapo Mijini
kuliko yale ambayo yapo Vijijini ambapo ndipo kwenye uitaji mkubwa sana kutokana na hali
ngumu ya maisha ambayo inafanya baadhi ya watu kwenda makanisani kwa msimu
Awali katika harambee hiyo vifaa mbalimbali vya ujenzi vilipatikana
sanjari na kiasi cha zaidi ya Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo la Amec wilayani
Meru Mkoani hapa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment