ACHENI MADHABAU ZA MABABU NA MABIBI ILI
MUACHANE NA UMASKINI NA MATESO YA DUNIA
Na Bety Alex,ARUSHA
MCHUNGAJI Mary Andrew wa kanisa la Victory Gospel Centre
liliopo Oltulelei Jijini hapa amesema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao
wanalia na umaskini katika maisha yao
ila bado hawajajua kuwa chanzo cha umaskini ambao wanao ni madhabau mbalimbali
ambazo walishawahai kuzitumikia au wanazozitrumikaia kwa sasa
Hili suala la Madhabau halibagui wala halichagui mtu yoyote yule anaweza kuyatumikia hata kama
ameokoa ili hali kama hajavunja na kuyakata
madhabau mbalimbali ambayo yanaendelea hapa duniani
Mchungaji Maria aliyasema hayo wiki iliyopita wakati
akionmgea na waumini wa kanisa hilo
kuhusu umuhimu wa kukataa kutumikia
miungu miwili ambayo ni kanisa pamoja na madhabau
Aidha alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao kila
siku wanalia nakuomba kukataa maroho
mbalimbali huku wakiwa wanatumia madhabau nyingine katika kuweka imani hali
ambayo inawafanya walio wengi sana
kuwa maskini
Alifafanua kuwa hali hiyo ya kutegemea zaidi madhabahu
kuliko Mungu ndio inayochangia kwa kiwango kikiubwa sana
watu wa leo kukosa haki zao za msingi kutoka kwa Mungu kwa kuwa imani zao
zimejengeka zaidi katika imani za kimadhabu kuliko kwa Mungu ambaye ndiye
tegemeo kubwa sana
‘ndani ya makanisa mpaka watu wanaokoka
na wanakiri kabisa
kumwamini kristo lakini nyuma ya mapazia wanakuwa wanamuamini zaidi
vibabu hasa
kwenye madhabau sasa hii ndio inayopelekea walio wengi sana
kuwa na mateso mbalimbali ikiwemo roho ya umaskini ambayo inatembeea
sana katika maisha ya wakristo hivyo nawasihi sana kuweza
kubadilika”alkiongeza
Mchungaji huyo
Katika hatua nyingine alisema kuwa wale wanaotumia madhabahu
mbalimbali wanakuwa katika ulimwengu miwili tofauti kwa kuwa
Kuwa madhabau hizo zinawaunganisha watu na kuzimu ambapo
ndipo kwenye chanzo kikubwa sana
cha mateso ya leo hapa duniani
‘biblia inaonesha hivyo kabisa kuwa zipo baadhi ya madhabau
ambazo zinaunganishwa na kuzimu na hizi
madhabau zimejengwa na mababu na mabibi sasa sisi watoto wa leo tunaoibukia
huko ndio tunaopata matatizo, majeraha, na mateso ya kudumu tunatakiwa
kuhakikisha kuwa tunaacha madhabahu hizo na kuangalia Kitabu cha Mithali 12
ambacho kinasema na kudai kuwa Mungu hana upendeleo kwa yeyote yule ambaye
anamtegemea”aliongeza
Alimalizia kwa kusema kuwa makanisa ya leo yanatakiwa
kuongeza na kuimrasisha nguvu zaidi katika kuwafundisha wakaristo wake umuhimu
wa kuyakimbia madhabahu na endapo kama makanisa hayatweza kufanya hivyo basi
yatakuwa yanachangia sana mateso na
manunguniko makubwa sana kwa maisha ya kila siku.
MWISHO
No comments:
Post a Comment