CHAMA cha wazee na wastaafu mkoa wa arusha( CHAWAMA)wameziomba
halimashauri zote za mkoa huo ziwasaidie uwanzishaji wa mabaraza ya
wazee kuanzia kwenye kata ili waweze kuunda baraza la wazee la wilaya
litakalowezesha kujadili mambo yao muhimu yanayowahusu.
Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa arusha
Elimirathi Mswia alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya wazee
duniani yaliyofanyika mjini hapa.
Mswia alisema kuwa wazee wa mkoa huu wanauhitaji mkubwa sana wa
kuanzishiwa baraza kuanzia kwenye kata ambapo amesema kuwa endapo
halimashauri zitawasaidia katika swala hilo ni wazi kuwa wataweza
kuunda baraza lao la wilaya ambalo litawasaidia kujadili mambo mbali
mbali yanayowahusu.
Alisema kuwa kuapatikana kwa baraza hilo wanalolihitaji itakuwa ni
moja ya hatua kubwa ambayo watakuwa wamefikia kwa kuwa mara nyingi
wanasdhindwa kufikia malengo yao wanayohitaji kwa ajili ya kutokuwa na
baraza lao maalum.
Mbali na hayo pia chama hicho kimeziomba halimashauri hizo kuweka wazi
bajeti za maswala ya wazee kwani kila mara wanapokwenda kwenye
halimashauri hizo kutafuta msaada hujibiwa kuwa hakuna bajeti hali
inayowafanya kutofikia malengo yao.
“sisi wazee tumekuwa hatuna bajeti yeyote katika halimashauri inafika
mahali unaenda kueleza shida zako ukiwa kama mzee lakini unaambiwa
hamna bajeti ya wazee kwanini na sisi tusiwekewe bajeti yetu na tuna
haki kama watu wengine?alihoji Mswia.
Kutokana na hali hiyo wameziomba halimashauri hizo kuweka maswala
yanayohusu wazee kwenye bajeti zao ili kupunguza ama kuondoa kabisa
adha wanazopata wazee hao pindi wanapoenda kuomba msaada huo sanjari
na kuwatafutia vitambulisho vya matibabu kwa kuwa bado hawapati huduma
nzuri za kiafya kutokana na halimashauri hizo kutowapatia vitambulisho
hiyvo.
Aidha waliiomba serikali ifikirie kwa mapana zaidi kuongeza kiwango
cha pensheni angalau kiweze kulingana na kima cha chini cha mshahara
wa wafanyakazi wa serikali maana kiwango chao hakiwatoshelezi
ilinganishwa na gharama za maisha zilivyopanda.
No comments:
Post a Comment