Na Queen Lema, ARUSHA
KAIMU mkurugenzi wa manispaa ya Arusha Bw Omary
Mkombole amewataka wananchi wa manispaa hiyo ambao wanaishi mabondeni kuhama
mara moja ili kuepusha majanga mbalimbali ya mafuriko ambayo yatatokana na mvua
kubwa za vuli ambazo ziunatarajiwa kuanza hivi karibuni
Bw Mkombole aliyasema hayo jana wakati akiongea
na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kupokea taarifa maalumu kutoka
mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA)ambayo ilidai kuwa mkoa wa
Arusha utakuwa na mvua nyingi sana
Alisema kuwa kutokana na taarifa hiyo wananchi
wanapaswa kuhama wenyewe tena kwa haraka sana
hasa wale ambao wanaishi katika maeneo ya mabondeni mwa manispaa ya Arusha
kwani endapo kama watakiuka hayo basi watasababisha sana maafa hasa nyakati hizo za mvua
kubwa
“Taarifa ambayo tumeipokea hapa inasema kuwa ni
lazima wananchi wachukue tahadhari mapema sana
kwani kutakuwa na ongezeko kubwa sana
la mvua zinazortarajiwa kuanza kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa huu na
kumalizika mwezi wa kumi na mbili hivyo hii ni amri ya Manispaa kuwa wananchi
hao wanatakiwa kuhama mara moja “alisema bw Mkombole
Hataivyo alitaja maeneo ambayo yanaweza
kukabiliwa na maafa ya mafurukio hasa nyakati za mvua kubwa ni pamoja na maeneo
ambayo yapo kwenye miteremko mikali, kwenye makorongo mbalimbali,ambapo kuanzia
sasa wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari ya kuhama maeneo hayo ambayo
wataalamu wamedai kuwa yana kabiliwa na hatari sana.
Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi huyo alisema
kuwa mbali na tahadhari ya mafuriko pia Halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha
kuwa Mji wa Arusha unakuwa na mpangilio wa hali juu hususani kwa
wafanyabiashara wadogo na wakubwa ambapo wanatakiwa kuuza bidhaa zao kwa
kufuata sheria mbalimbali za majiji ya Kimataifa duniani
Alisema kuwa kwa sasa Manispaa hiyo itahakikisha
kuwa tatizo la uuzwaji wa bidhaa unafuatwa kwa haraka sana
ambapo wafanyabishara wote wanatakiwa kuuza bidhaa zao ndani ya maduka yao sanjari na kutumia Mabohari ili kuufanya mji wa Arusha
kuwa katika kiwango cha usafi wa hali ya juu sana
No comments:
Post a Comment