Na Queen Lema, Arusha
TANZANIA KUENDELEA KUBORESHA HIFADHI ZA UTALII PAMOJA NA VYANZO VYA MAZINGIRA
SERIKALI ya Tanzania
imesema kuwa itaendelea kuweka na kuimarisha mikakati mbalimbali ya mazingira
pamoja na utalii ambapo mikakati hiyo itaenda sambamba na kuzuia makazi ya watu
karibu na vyanzo mbalimbali vya mazingira na hifadhi kwani makazi hayo ni
tishio kubwa sana
kwa wanyama
Hayo yameelezwa na Makamu wa Raisi Dkt Gharib Bilal wakati
akifungua Kongamano la kwanza la usimamizi endelevu katika hifadhi za taifa
mapema leo jijini hapa
Dkt Bilal alisema kuwa mikakati hiyo itafanya baadhi ya
wananchi kushindwa kukaa karibu na vyanzo na hifadhi za wanyama kwa kuwa
asilimia kubwa ya makazi ya watu yamekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira pamoja
na vifo vya wanyama hasa Tembo hali ambayo inafanya malengo mbalimbali ya
uhifadhi kushindwa kutimia
Aliongeza kuwa pamoja na kuweka mikakati hiyo lakini bado
suala hilo limekuwa ni gumu sana kwa wananchi kwa kuwa baadhi ya
wananachi ambao wanafukuzwa katika vyanzo
vya mazingira wanagoma kuondoka huku idadi ya wanyama nayo ikiwa
inapungua kutokana na makazi hayo
“tuna mikakati ya kuhakikisha kuwa maeneo ya hifadhi ya
taifa na vyanzo vingine vya mazingira
vinahifadhiwa na kamwe maeneo haya yasiingiliwe kwa ajili ya makazi ya kudumu
ya watu ambapo kama tutafanikiwa kufanya hivi basi tutachangia sana kwa kiwango
kikubwa kuongeza hata idadi ya wanyama
hasa Tembo ambao wamepungua sana ndani ya hifradhi mbalimbali za Taifa hapa
nchini”aliongeza Dkt Bilali
Awali Naibu katibu mkuu wa shirika la umoja wa mataifa
linalohuisiana na utalii(UNWTO)bw Hifad Twalib
alisema kuwa utalii unatakiwa kuanzia ngazi ya chini na endapo kama
wananchi wa nchi husika hawafurahii utalii basi utalii huo utakuwa hauna maana
halisi hasa kwenye mapato.
Aliwataka wananchi wan chi zote hasa kwa bara la Afrika
kuhakikisha kuwa wanayafuraia mazingira ya utalii na kuhakikisha kuwa wanakuwa
mabalozi wazuri hali ambayo kama itafanikiwa kuboreshwa
basi hata idadi ya vyanzo mbalimbali vya utalii navyo vitaongezeka kwa kuwa
baadhi ya vyanzo vya utalii vinakufa kwa kuwa hakuna uhamasishaji mkubwa.
‘sasa unakuta nchi inatangaza utalii wakati wananchi wake
wenyewe hawajui na kwa kweli hili ni
suala gumu sana wananchi wanatakiwa kubadilika na kuhakikisha kuwa kabla ya
wageni kutoka nje ya nchi hawajaja wananchi wenyewe waweze kuutambua na
kuthamini utalii nah ii itasababisha sana wananchi kuweza kunufaika sana na
hata kuutangaza utalii wao wenyewe’aliongeza
MWISHO
No comments:
Post a Comment