MWENDESHA MASHITAKA, MAWAKILI WA UTETEZI WAKATA RUFAA KESI YA LUBANGA
Na Hirondelle,Arusha
Arusha,
Oktoba 05, 2012 (FH) – Pande zote mbili, za utetezi na mwandesha
mashitaka katika kesi ya kiongozi wa zamani wa wanamgambo katika Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga, zimekata rufaa kupinga
adhabu aliyopewa mshitakiwa huyo ya kifungo cha miaka 14 jela.
Mahakama
ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyopo The Hague Uholanzi, Julai
10, 2012 ilimtia hatiani Lubanga kwa uhalifu wa kivita kwa kuwasajili
na kuwatumia watoto katika mapigano eneo la Ituri, Mashariki mwa DRC
kati ya Septemba 1, 2002 na Augosti 13,2003. Wakati huo Lubanga alikuwa
kiongozi wa kundi la waasi la UPC.
Wakati
mwendesha mashitaka anapinga adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela
akitaka iongezwe, upande wa utetezi unapinga vyote viwili, kutiwa
hatiani na adhabu aliyopewa.
Lubanga
alitiwa mbaroni Kinshasa mwaka 2005 na kisha kuhamishiwa ICC, The Hague
March 2006. Kesi yake ilianza kusikilizwa Januari 26, 2009.
ICC,
ambayo ni mahakama pekee ya kudumu duniani ya kushughulikia kesi za
mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu
imeshotoa hati kadhaa za kukamatwa kwa wahalifu wa makosa kama hayo
nchini DRC.
Nje
ya Lubanga, wengine walioshitakiwa pia mbele ya mahakama hiyo ni pamoja
na viongozi wengine wawili wa wanamgambo, Germain Katanga na Mathieu
Ngudjolo ambao wanasubiri kutolewa kwa hukumu za kesi dhidi yao.
No comments:
Post a Comment