Monday, October 29, 2012

DKT BILALI AVITAKA VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI KUFIKIRIA ZAIDI AJIRA KWA WAHITIMU WAO

MAKAMU WA RAISI WA TANZANIA DKT GHARIB BILALI AKISISITIZA JAMBO KWA WADAU WA MKOA WA ARUSHA HIVI KARIBUNI


Na Queen Lema,ARUSHA


 MAKAMU wa Raisi Dkt GharibBilali amevitaka vyuo vikuu mbalimbali kwa nchi za Afrika mashariki kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kufikiria maitaji ya wahitimu hasa Upande wa ajira hali ambayo itasaidia sana kuweza kupunguza tatizo hilo            kwani kwa sasa asilimia kubwa ya vyuo vinazalisha bila kufikiria aina ya masoko ya ajira kwa wahitimu wao.

Dkt Bilali aliyasema hayo jana wakati akizundua mkutano wa kwanza ambao unaounganisha Umoja wa vyuo vikuu na umoja wa wafanyabiashara kwa nchi za jumuiya ya Afrika ya Mashariki

Alisema kuwa kwa sasa ndani ya nchi za Afrika ya mashariki kilio kikubwa sana ni ukosefu wa suala zima la ajira hali ambayo inafanya malengo mbalimbali kushindwa kutimia

Aliongeza kuwa endapo kama vyuo hivyo vitaweza kushirikiana kwa pamoja basi na kuangalia maitaji ya wahitimu basi vitachangia kwa kiwango cha hali ya juu sana maslahi mazuri kwa wahitimu pamoja na nchi husika

“kama wamiliki wa  vyuo wataweza kufanya hivyo mapema na kuangalia kwa undani sana tofauti na pale ambapo wanatoa wahitimu bila kuangalia suala zima la  mahitaji ya wahitimu basi hata hali ya elimu kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki utaweza kuongeza hata idadi ya wasomi bora ambao wataweza kusaidia jamii husika’aliongeza Dkt Bilali


Pia alisema kuwa nazo nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu mzuri wa kusaidia na Vijana ambao  ni wahitimu na kuweza kutumia ujuzi ambao wameupata tofauti na pale ambapo wanaposhindwa kutiumia ujuzi wao kwa kisingizo cha ukosefu wa ajira ilihali bado jamii inakabiliwa na changamoto na uhaba wa wataalamu mbalimbali

“ushirikiano ni muhimu sana kwani baadhi ya watu wanakwepa hawa wahitimu ilihali jamii zao zinakabiliwa na mambo mbalimbali sasa ni vema kama kila jamii ikahakikisha kuwa kila muhitimu anakuwa na sehemu ya kwenda mara baada ya kuhitimu elimu ya juu na elimu aliyoipata ianatakiwa kutumika ili kuongeza ufanisi zaidi kwa nchi zetu za Afrika ya mashariki”aliongeza Dkt Bilali.

Katika hatua nyingine alisema kuwa endapo kama kutakuwa na umoja baina ya jamii ,wahitimu wa vyuo vikuu, na wafanyabiashara uchumi wa nchi za Afrika ya Mashariki utaweza kuoboreka sana na kuweza kuvuka viwango mbalimbali ambavyo vinasababishwa na uhaba wa wataalamu wa kutosha

MWISHO

No comments:

Post a Comment