Na Queen Lema,ARUSHA
ZAIDI ya wakazi 6000 kutoka katika kata ya
daraja mbili mkoani hapa wanatarajiwa kufikiwa na elimu ya mazingira ingawaje
kwa sasa bado mitaa mbalmbali ya Kata hiyo inaongoza kwa uchafu na
uharibifu wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vyanzo vya maji hali ambayo inachangia
mlipuko wa magonjwa na ukame
Hayo yameelezwa jana na mtatibu wa shirika la
Initiative for youth(INFOY) bw Laurent Sabuni wakati akiongea na wananchi wa
mitaa mbalimbali ya Kata hiyo ambayo bado inakabiliwa na tatizo kubwa la
uchafuzi wa mazingira kutokana na uhaba wa elimu ya utunzaji wa mazingira
Bw Laurent alisema kuwa wananchi hao
watafanikiwa kupatiwa elimu kuanzia sasa ambapo elimu hiyo italenga kufanya
kata hiyo kuwa katika hali ya usafi kwani kwa sasa hali ya usafi katika kata
hiyo ni mbaya sana hususani kwa nyakati kama hizi ambazo Mvua zinatarajiwa kuanza kwa wakati
wowote ule.
Alisema kuwa wamelazimika kutoa elimu hiyo ili
kufanya kata hiyo na mitaa yake kuwa na usafi wa kutosha ilin kuepusha madhara
mbalimbali ambayo yanajitokeza kutokana na uchafu uliokithiri pembezoni mwa
barabara na hata katika vyanzo mbalimbali vya maji hususani Mito ambayo inazunguka kata hiyo
“tumelezimika kushirikiana na wenzetu wa
Foundation for Civil Society kuweza kuokoa afya za watu hawa 6000 ambao miongoni
mwao wapo watoto kwani hali ya usafi bado ni ndogo sana ingawaje kwa sasa
Jiji linahimiza kufanya hivyo sasa kwa hiyo hawa watakaopata elimu hii
tunatarajia kabisa wataweza kufanya mabadiliko makubwa sana”aliongeza Bw
Laurent
Pia alisema kuwa ili kuhakikisha zoezi hilo la kuokoa maisha ya watu wa kata hiyo ya daraja mbili
linafanikiwa kwa kiwango kikubwa pia wamefanikiwa kujiwekea taratibu mbalimbali
ambazo zitatumika kulinda mazingira mbalimbali ya Kata hiyo ambapo taratibu
hizo zitawafanya wachafuzi wa mazingira kuepukana na tabia hiyo kwa kuhofia
kufikishwa mahakamani na kutozwa faini kubwa sana
Alibainisha kuwa nazo kata nyingine zinatakiwa
kuhakikisha kuwa zinakuwa na sheria kali sana hasa kwa wachafuzi wa mazingira
kwani bado jamii inakabiliwa na watu hao kwa kuwa wanafikiri kuwa sheria
hazipo na kama zipo hazitekelezwi huku hali ikisababisha baadhi ya mitaa ya
Jiji la Arusha kukithiri kwa kiwango kikubwa sana cha uchafu
“Mitaa kupitia Serikali zake zinatakiwa
kuhakikisha kuwa sheria mbalimbali za utunzaji wa mazingira zinafutwa lakini kama sheria zitakuwa zinawekwa maofisini pekee na
kushindwa kufafanuiliwa kwa wananchi huku hali ikisababisha baadhi ya watu
kutumia fursa hiyo kuchafua mazingira ovyo na kufanya hata jitiada mbalimbali
za wadau wa mazingira kushindwa kutekelezwa kwa wakati”alisema Bw Laurent
No comments:
Post a Comment