TUME YA TAIFA YA KUDHIBITI UKIMWI YATAKIWA KUANGALIA MAKUNDI MAALUMU
Na Queen Lema,ARUSHA
TUME ya
taifa ya kudhibiti ukimwi, TACAIDS, imetakiwa
kuangalia makundi maalumu ya kijamii
kwa kuyafuata huko yaliko ili kuyapatia elimu ya kuepukana na ukimwi
badala ya kuyaacha yakiendelea
kusambaza na kuueneza na hivyo
kufanya mapambano ya kuudhibiti na kupunguza ukimwi kuwa ngumu.
Rai hiyo
imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, katika hotuba ya
ufunguzi ya warsha ya siku tatu iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Deus
mnasa,kuhusu mpango mkakati wa awamu ya
tatu wa mpango wa taifa wa miaka mitano ,2008/ 2012 na 2013 hadi 2017 .
Warsha hiyo
inashirikisha wadau mbalimbali ambao ni wawakilishi wa Sekta ya Utalii,
wafugaji , mashirika yasiyo ya kiserikali, wachimbaji madini, waishio na virusi
vya ukimwi, asasi za kijamii, maafisa maendeleo ya jamii,maafisa mipango wa
wilaya, na afisa uchumi kutoka Sekretariet ya mkoa wa Arusha , waratibu wa
ukimwi wa halmashauri za wilaya kutoka
mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara .
Mkuu wa
mkoa, amesema kwa kuwa semina hiyo inalenga utambuzi wa mahitaji ya watu walioko katika hatari ya
kupata maambukizi mapya ya virusi, tume
inatakiwa kuwafuata wale wote wanaojihusisha na ngono kwenye madanguro ,sanjari
na vijana na kuwapatia elimu ya kujikinga na ukimwi kwa sababu ni makundi
muhimu ya nguvu kazi.
“Maambukizi
yatapungua iwapo tu makundi maalumu yakiwemo ya vijana na wasichana wanaofanya
ngono katika madanguro watapatiwe elimu badala ya kuwaacha pembeni bila ya
kuwasaidia”alisema magesa..
Magesa,
ameitaka ,Tacaids, kutafuta utaratibu
mzuri wa kuliandalia program maalum
kundi linalofanya biashara ya ngono kwenye madanguro ili kuzuia ngono za hovyo
ambazo zimeenea katika miji mbalimbali nchini ili kuliepusha lisipate maambukizi na kusambaza ukimwi kwa wengine kutokana na
kutokuwa na elimu ya kujikinga na kuchukua tahadhari.
Tacaids
ianzishe mpango wa kuwawezesha walioathirika na ukimwi kuanzisha miradi ya
kiuchumi ili waweze kujiajiri na
kuachana na utegemezi na omba omba hali
ambayo inasababisha vifo vya haraka..
Pia Tacaisd,
ihakikishe fedha za misaada zinazotolewa kwa waathirika na wagonjwa kupitia
mashirika na asasi za kijamii zinawafikia walengwa ,badala ya watoa huduma ambao
wanajinufaisha kwa kununua magari ya
kifahari na kujenga nyumba huku walengwa
wakiwa hawanufaiki .
Magesa,
ameitaka Tacaids, kutumia tafiti za kitaalam
kuhusu ukimwi ziweze kusaidia kupunguza kiwango cha maambukizi badala ya
tafiti hizo kubakia kwenye makabati bila kufanyiwa kazi na hilo ni jambo la
kusikitisha na kushangaza.
Amesema
iwapo Tacaids itatumia tafiti hizo
maambukizi mapya ya ukimwi ,ni wazi kuwa maambukizi yatapungua na hivyo kuondoa unyanyapaa na vifo tatizo ambalo limekuwa likizikabili jamii mbalimbali hapa nchini.
“Umefika
wakati Tacaids, kuaandaa utaratibu utakaowawezesha waathirika na wagonjwa wa ukimwi kupata hati
miliki ya mali zao ili kuepuka kunyang’anywa pindi wenza wao wanapofariki kutokana
na mila potofu ambazo ni kandamizi zimekuwa zikiwanyima haki wajane badala ya
kuwaacha waendelee kuishi kwa matumaini” alisema magesa.
Amezitaka Kamati za ukimwi katika halmashauri zishirikiane kikamilifu ili kupunguza
maambukizi ya ukimwi ,kwa kuwa ukimwi ni vita
ya kibailojia iliyoletwa kwa
ajili ya kudhoofisha ukuaji wa uchumi katika mataifa yanayoeendelea.
Amesema
serikali inataka kuwepo thamani halisi ya utekelezaji wa mpango wa mkakati wa
mapamano ya ukimwi
Magesa,ameitaka
tacaids, kutambua kwa nini maambukizi ya ukimwi yanaendelea kusambazwa kutokana na vijana kujiingiza kwenye mapenzi
wakiwa katika umri mdogo ,umaskini wa familia na kutokulelewa kimaadili .
Amesema
Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano ya Ukimwi kutokana na kuwa na
sera nzuri na mkakati wa makusudi hivyo Tacaids iongeze kasi zaidi na iangalie
uwezekano wa kutoa elimu ya ukimwi kwenye vyuo vikuu ambako maambukizi yapo juu
na kuliokoa kundi hilo ambalo limeaachwa .
No comments:
Post a Comment